Zijue Mbinu Zangu za 'Negotiation'

Zijue Mbinu Zangu za 'Negotiation'

Mc cane

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
5,570
Reaction score
10,517
Habari za mida hii wakuu

Kama kawaida, pamoja na mambo mengine tumekuwa tukitumia majukwaa mbalimbali katika forum kwa malengo tofauti tofauti. Elimu ni moja kati ya malengo hayo, leo tuangalie elimu inayogusa maeneo mengi lakini hususani kwenye biashara.

Ni ukweli usiopingika kwamba kila saa, kila siku, karibu kila mahali tunafanya 'negotiation'. Ukiomba kazi unafanya 'negotiation' na bosi kwenye masilahi yako, ukienda dukani unafanya 'negotiation' upunguziwe bei, ukinunua kiwanja unafanya 'negotiation' ulipe kwa instalments 2 kwa mwaka au 3 au 4 ili mradi usiumie kwa upande wako. Mwezi June hadi July kuna wanandoa walifanya 'negotiation' kuwa mke ashike remote ya television asubuhi tu na mme ashike remote kuanzia alasiri. Marekani amekuwa akifanya negotiation mara kadhaa na nchi kama Iran na Korea Kaskazini kuhusu suala la Nyuklia. Hiyo ni mifano michache tu.

Kabla ya kusema mengi niseme tu kwamba 'Negotiation' ni somo kabisa katika vyuo, hivyo nitakachoeleza hapa ni kama tone tu baharini ili kusaidia ufahamu kuhusu hili suala.

Ku 'negotiate' ni kufanya makubaliano ambayo kila upande unataka upate/unufaike zaidi katika kile kinachozungumziwa. Baada ya kupata utangulizi twende kwenye mbinu zangu ninazotumia kufanya 'negotiation'.

1. Nafanya maandalizi kabla ya kwenda kufanya hayo makubaliono.
Hapa ninangalia alternatives nilizonazo endapo hatutafikia muafaka na mwenzangu. Ninaangalia alternatives alizonazo mwenzangu. Kwa kuangalia hivyo nitajua ninambana vipi huyu mwenzangu. Akiwa hana alternatives nyingi au hana kabisa basi hapo ndio pa kupata lion share.

2. Ninazingatia niwe wa kwanza au wa mwisho wakati gani kutoa offer yangu.
Kama nikiwa nina taarifa za kutosha kuhusu upande wa mwenzangu mfano alternatives alizo nazo,yupo tayari kulipa/kuuza kwa shilingi ngapi n.k nitakuwa wa kwanza kuweka ofa. Kama sina taarifa za kutosha nitasubiri aanze yeye.

3. Ninaangalia zaidi nguvu/uzaifu wake katika kufanya makubaliano.
Ninajiuliza atafanya nini/Atakosa nini haya makubaliano yakishindikana badala ya nitafanyaje endapo tusipokubaliana. Siongei hovyo hovyo,ninakuwa msikilizaji zaidi,ukimya wakati wa 'negotiation' ni mbinu mojawapo. Mtajie mwenzako hasara unayopata baada ya kukubali ile kwako,hii ita saidia kumfanya na yeye aone kuna haja ya kukubali ile kwake pia.

4. Hata nikiona ofa ya mwenzangu ni nzuri sana kwangu simuoneshi kwa kukubali haraka haraka. Kuchelewa kukubali itanifanya mimi na mwenzangu wote kuwa na furaha baada ya 'negotiation' kumalizika.

5. Huwa sijiulizi tu NINI?Pia huwa najiuliza KWANINI?
Kwanini bei kubwa sana,kwanini bei ndogo sana,kwanini hataki kuuza? Pengine hataki kukuuzia kiwanja kwa milioni 10,na anng'ang'ania milioni 20 sababu ya ugumu wa kupata kiwanja kingine. Vipi ukimwambia unamlipa milioni 8 halafu utampa kiwanja kingine (ambacho wewe umekinunua kwa milioni 2? ).

6. Natumia njia mbalimbali kupata taarifa za mwenzangu
Mfano,najenga imani kwa ku share nae baadhi ya taarifa,namuuliza maswali yasiyomtisha,ninataja mambo mbalimbali mengi katika Ku negotiate, hii inasaidia kujua vipaumbele vya mwenzangu ili nijue pa kumbana.

7. Naangalia mambo mengine,na si bei tu.
Ninaangalia pia interests za mwenzangu. Pengine anapenda sana maeneo tulivu,hivyo japo Nina eneo mbali na mji lakini kwake lina thamani kubwa, hivyo nitambana tu kwenye bei.

8. Najitahidi kudhibiti hisia kipindi ninafanya negotiation.
Unaweza kuwa na kesi ambayo itagharimu Tsh 20,000/= lakini ikafika 1,000,000/= eti kisa kila upande unataka haki.

9. Siku zote nataja kikubwa zaidi ya kile ninachokitaka au nataja kidogo zaidi ya kile nilichoombwa

10. Sidanganyi (unethical), ila sijibu swali mja kwa moja, au natafuta namna ya kupotezea

Hizo ni baadhi ya mbinu zangu kwenye negotiation,mbinu zako ni zipi?
 
Umeandika vyema mkuu, Negotiation ni somo la msingi sana ktk maisha ya biashara na ujasiriamali.

Kwenye kitabu cha ART OF THE DEAL kilichoandikwa na Donald Trump kimeelezea pia kuhusu suala hili.

Naongezea kuwa kabla haujaanza negotiation ya deal yoyote hakikisha kwanza unafahamu vyema kuhusu kitu/biashara mnayokubaliana kama hufahamu vizuri basi tumia wataalamu wa suala hilo.


TUSOMENI VITABU JAMANI VINATUSAIDIA SANA.
 
Hili somo wanawake by default wamezaliwa nayo.
Wanaume huwa tunajikuta wenyewe tunatoa hela.
 
Umeandika vyema mkuu, Negotiation ni somo la msingi sana ktk maisha ya biashara na ujasiriamali.

Kwenye kitabu cha ART OF THE DEAL kilichoandikwa na Donald Trump kimeelezea pia kuhusu suala hili.

Naongezea kuwa kabla haujaanza negotiation ya deal yoyote hakikisha kwanza unafahamu vyema kuhusu kitu/biashara mnayokubaliana kama hufahamu vizuri basi tumia wataalamu wa suala hilo.


TUSOMENI VITABU JAMANI VINATUSAIDIA SANA.
Ni kweli mkuu
 
Back
Top Bottom