Zijue MISSION 09 za KBG (FSB sasa) ambazo kama baadhi zingefanikiwa Dunia ingekuwa tofauti na leo



Mkuu MSEZA MKULU ,
Shirika la KGB lilivunjwa na kuwa SVR na FSB mara baada ya kuanguka kwa jumuiya ya nchi za kisovieti mwaka 1991 na siyo mwaka 1995.

Haya nianze kukosoa kwenye vinasa sauti hapo.
Hivi unajua mnamo mwaka 1970 C.I.A walichimba shimo refu chini ya Ubalozi wa Soviet Marekani kwa dhumuni la kufanya udukuzi?

Hilo la ugaidi.
Mbona C.I.A na MOSSAD nao ni magwiji wa kutengeneza magaidi?
Unayakumbuka haya makundi;

  1. Khmer Rouge la Cambodia?
  2. Contras or FDN wa Nicaragua?
  3. The Mujaheddin au Al-Qaeda la Afghanistani?
  4. Hawa ISIS je?
 
mkuu hiyo svr -rf ndio ilianzishwa 1991. Lakini April 1995 rais wa Urusi Boris Yeltsin alisign sheria iliyofanya kuanzishwa officially kwa FSB. Zama kidogo mkuu. Lakini zote ni taasisi za kikachero zilizosambaza maelfu ya watu dunia nizma kama ilivyo CIA na Mossad.

Kuhusu ugaidi tuko pamoja kabisa. Ila kwenye hiyo list nitafuatilia nipate ujuzi wa mambo maana elimu haina mwisho.
Source za IRNA (iranian media) na mdukuzi snowden wanasema Kiongozi na muanzilishi wa ISIS AL BAGDAD ni MOSSAD Highly trained, na lengo ni kudhoofisha maadaui wa israel ili wao waishi kwa amani.

haya mambo ni magumu wengine huwa tunapenda kufuatilia kama burudani maana yanasisimua na kufikirisha.
 
CIA & FBI kuna tofauti gani?
FBI ni domestic agency. wao wanafanya kazi ndani ya US tu. Ila CIA mkuu hawa kazi kubwa ni nje ya marekani, na hawaruhusiwi kufanya upererezi ndani ya US maana huko wapo FBI ingawa wanaweza kushirikiana baadhi ya mazingira. CIA wamesambaa dunia nzima wao na informers kibao wanao report kwao na wako nyuma karibu ya kila kitu kinachoendelea kila kona ya dunia.
mfano: warusi wanalaumu hata anguko la rais wa FIFA kwa kashfa za ufisadi CIA wako nyuma ya tukio.
 

FSB lilikuwepo,
Kabla ya 1995 ilikuwa inaitwa FSK (Federal Counter Intelligence Service),
Ilikuwa inaongozwa kwa amri ya raisi (President's decree); mwaka 1995 ikapitishwa sheria na bwana Putin akawa Mkurugenzi.

Ni sawa na kusema TIS na TISS kabla ya mwaka 1997,
FSB si shirika la nje.
SVR na GRU ndiyo mashirika ya nje.
 
Umemjibu vizuri. FBI ni shirikisho la kikachero la ulinzi wa ndani ya US ingawa wanaweza kwenda popote duniani kufuatilia suala lililo ktk mipaka ya majukumu yao
 
 
Ahsante mkuu umenifumbua macho haya mambo nayapenda sana kuyafuatilia maana ni burudani kwangu.
 
yap tuko sawa, hiyo ndiyo ilikuwa maana yangu 1995.
Tuko pamoja
 
Mbona TISS siioni hapa mwoshoni walau?
 
Tiss hamna ishu sifa nyingi, ukiwa hata bar mtu anakwambia mie usalama... siku hizi hawana siri
Bora hao wanajitangaza bar Mbona hao FBI wanavaa kabisa vizibao vyao wala haihitaji mtu kwenda kusikiliza,japo kuna wasiovaa pia kama wale wa TISS nao wasio jitangaza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…