Dogoli kinyamkela
JF-Expert Member
- Nov 21, 2024
- 618
- 1,440
ZIJUE NYAKATI VIZURI (1)
Imeandaliwa na kuandikwa na Dr Dogoli kinyamkela
🗣️Kila kiumbe ambacho kinaishi katika dunia hii kina nyakati zake, majira yake ya kuwa hivi ama vile Kulingana na nyakati husika ya hicho kiumbe.
✍️Nyakati au muda ndiyo unafanya tuweze kuyachanganua matukio, na matukio ndiyo yanafanya tuuthamini au tuelewe Kama nyakati zipo.
🌄Na hapa duniani kwa vile tuko katika mfumo wa Sola system hivyo hatuwezi kukaa mbali na nyakati.
🤗Kuna rafiki yangu mmoja alinifuata Nyumbani huku akiwa mwingi wa huzuni, akaniambia kwamba mke wake ameondoka Tena kwa kejeli Sana, akawa anataka nimsaidie ili tuweze kukiskip hiki kipindi na siyo tu mke wake kuondoka Bali hata maisha yake Sasa yamekuwa magumu Sana.
🙄Kitu ambacho rafiki yangu alishindwa kuelewa kwamba matukio ndiyo yanayofanya tuone nyakati zipo maana hapa utalinganisha kipindi kile na hiki.
😂Embu tuachane na habari za rafiki yangu Basi turudi kwenye mada yetu maana mko makini kunisikiliza mkasa wa rafiki utafikili huyo rafiki ninaye kweli😂😂.
🗣️Sasa tuje kwenye mada yetu, nyakati zimegawanyika sehemu kuu tatu, Kuna wakati uliopita, uliopo na ujao.
✍️Lakini katika hizi sehemu tatu sehemu muhimu kabisa kuliko zote Ni huu wakati uliopo, endelea kunisikiliza utaelewa kwa Nini.
👍Hapa katika wakati uliopo ndiyo sehemu pekee ambayo tunaweza kutengeneza nyakati zote tatu, maana ukifanya vibaya katika wakati huu uliopo hapo utakuwa umeiharibu future yako mpaka past yako, vipi bado nimekuacha au.
✍️Ukija kwenye mathayo 6:34 nao unasema
🗣️Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
🤫Kama utakuwa makini hapa yesu alikuwa anazungumzia nguvu ya nyakati japo kwa uficho Sana, ninaposema nguvu ya nyakati namaanisha Ile sheria au kanuni ya sababu na matokeo yake, yaani kila matokeo unayoyaona yalikuwa na sababu yake huko nyuma.
🗣️Nyakati Ni mfano wa shamba ambalo kabla ya kuvuna kutakuwa na hatua zake ambazo Ni kuandaa shamba, kupanda mbegu na mwisho kuvuna.
🖐️Wakati wa Sasa ndiyo wakati muhimu Sana wa kuhakikisha unafanya lile lililo sahihi bila kuangalia matokeo yatakuwaje wewe fanya tu lililo sahihi matokeo yatakuja tu Kulingana na hiki unachokifanya.
🤫Usikate tamaa eti nimefanya kwa siku tatu au wiki Halafu hakuna majibu wewe usiangalie majibu wewe fanya tu Jambo sahihi Sasa muda wa kuvuna ukifika Basi utapata majibu Kulingana na kile ulichokifanya.
✍️Kama Leo ukifanya Jambo sahihi Basi matokeo yake yatakuwa mazuri kwako na Kama ukifanya Jambo tofauti matokeo yake yatakuja kuwa tofauti pia.
🗣️Hii Hali uliyo nayo Leo Ni matokeo ya Yale uliyoyafanya siku zilizopita, Na matokeo ya siku zijazo yanategemea Sana kile ambacho unakifanya leo.
Ulikuwa nami mwalimu wako Dogoli kinyamkela.