6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Niaje waungwana
Kwanza kabla ya kuelezea sababu za jeshi letu kutokutoa kichapo kwa M23, naomba kwanza nianze kuwapa historia tukufu ya jeshi letu la JWTZ au TPDF kwa nchi mbali mbali za Africa na Dunia kwa ujumla.
JTWZ chini ya baba wa taifa letu hayati mwl. Julius K. Nyerere ndio iliyoongoza mapambano yasioshindwa ambayo kwa asilimia kubwa yalisaidia nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Namibia na Angola kuwa katika mikono salama, na amani ya kudumu mpaka leo.
Idi Amin alitaka kujichanganya eti aichukue Bukoba, matokeo yake imechukuliwa nchi yake mwenyewe, halaf yeye akatoka nduki.
JWTZ hiyo hiyo chini ya utawala wa hayati mzee Ally Hassan Mwinyi ndio iliyotoa kichapo kitakatifu kwa jeshi la Burundi ambalo lilitaka kuteka sehemu ya mkoa wa Kigoma, kwa kisingizio cha kuja kuwapiga waasi wa CNDD-FDD ambao walikuwa wakipambana na serikali ya Burundi chini ya uongozi wa raisi meja Pierre Buyoya (rip).
Ni kwamba Buyoya na serikali yake walikuwa wanadai kwamba serikali ya Tz imekuwa ikitoa msaada wa kuwahifadhi waasi hao katika maeneo ya mpakani mwa Mkoa wa Kigoma na Burundi. Hivyo dawa ya kukomesha jambo hilo ilikuwa ni kuivamia Tz (Buyoya sijui nani alimhadaa ashike moto kwa mkono), kuichapa na kuteka maeneo yote aliyodai yanatumiwa na waasi nchini kwetu kufanyia training na kupanga mipango ya kuingia Burundi kufanya maangamizi mara kwa mara.
Soma, Pia: Askari wawili JWTZ wafariki dunia, wanne wajeruhiwa mashambulizi ya M23 huko Goma, DRC
Basi bwana Buyoya akaamuru jeshi lake lifanye ambush kupitia mipaka ya ardhini na majini. Aisee kilichotokea kwa upande wa Burundi mpaka leo ni hasara kwa nchi yao.
Kuna jamaa fulan Mrundi anasema kuwa sehemu hiyo iliyoangukiwa na kombora kutoka Tz mpaka sasa hapajawahi kuota chochote, na wala kujengwa chochote. Ni kama vile ardhi imeunguzwa hata kwa kutumia kutengenezea tofali za kuchoma haifai kudadeki. Baada ya lile tukio Buyoya na warundi wenzie wakawa wapole na askari waliokuwa wanalinda mipaka ya majini na ardhini kwa upande wa Burundi akawasogeza mbali mno kutoka mpakani.
Chini ya utawala wa raisi Kikwete kuna raisi alikuwa ashapinduliwa hapo Comoro, ikabidi aje kuomba msaada wa kumrudisha madarakani. Ni kitendo cha masaa tu raisi akarudishwa na wahuni waliopanga mapinduzi wakatiwa nguvuni.
Pia chini ya Kikwete raisi wa Burundi hayati Pierre Ngurunziza alikuwa ameshapinduliwa na kuambiwa abaki huku huku Tz alipokuwa amekuja kwa mkutano wa amani. Baada ya ujinga huo, Kikwete akatuma kikosi kidogo tu cha wanajeshi wa kumrudisha nchini kwake salama na kuwatia nguvuni wapuuzi wachache waliompindua raisi wao. Bila kuchelewa jeshi letu likamrudisha Ngurunziza, ila wapinduaji wakafanikiwa kutoroka na kukimbilia nchi jirani.
Chini ya utawala huo huo wa Kikwete jeshi letu lilitoa kipondo ambacho kilisababisha waasi wa M23 kutimkia Uganda na Rwanda. Na hii ni baada ya raisi wa Rwanda mhe. Paul Kagame kumletea dharau Kikwete na jeshi letu hali iliyosababisha Kikwete adili na kila kinachompaka Kagame jeuri. Alianza na wanyarwanda waliokuwa wanaishi nchini kinyume cha sheria, baadae akarukia Congo kuwafyeka M23 ambao waliaminika kuwa ni jeshi dogo la Rwanda. Kisha akasogeza jeshi mkoa wa Kagera kuwa tayari kuingia Kigali, sema hekima Za mzee Mwinyi na Mkapa zilichangia kumfanya Kikwete asivaamie Rwanda kumtoa adui yake.
Tukiachana na hayo. Tushapandikiziwa vikundi vya waasi kwa mgongo wa dini huko Tanga, Kibiti nk. Lakini jeshi letu halijawahi kucheka na kima wote tumewaangamizi kwa muda mfupi sana.
Hizo operations zote nilizoeleza hapo juu zilitekelezwa na TPDF bila kushindwa wala kurudi nyuma. Hivyo uwezo wa kumpiga adui toka miaka hiyo tulikuwa, tunao na tutaendelea kuwa nao. Huu ndio ukweli halisi.
Sasa tukija kwa hii vita ya sasa ya M23. Kuna watu wanajiuliza iweje M23 hii tulioichapa wakati wa Kikwete imetushinda wakati wa Samia!!
Ukweli ni kwamba jeshi letu lipo imara, vizuri na tayari kwa mapambano wakati wowote bila kujali ni nani aliepo madarakani. Kikubwa ambacho hufanyika ni kuliongezea jeshi silaha za kisasa, mbinu mpya za kijeshi, nguvu na morali zaidi za kulitumikia jeshi la wananchi. Pia jeshi letu hupambana kupitia amri ya amiri jeshi mkuu na wasaidizi wake. So kama amiri jeshi mkuu haoni tija yoyote ya jeshi letu kupambana huko Congo na kwengine basi jeshi letu halitopambana.
Sasa kinachoendelea Congo kwa sasa ni tofauti na kile kilichokuwa kinaendelea kipindi kile cha 2013 hadi 2014. Kipindi kile tuliingia vitani kivita kweli kweli, huku amiri jeshi mkuu wa Tz akiwa na lengo la kumshikisha adabu amiri jeshi mkuu mwenzake wa nchi jirani. Hivyo ilikuwa ni vita ya serious ndiomaana tuliwachapa M23 bila huruma hadi wakakimbia wenyewe na kuacha silaha zao.
Lakini hii vita ya sasa hivi Congo sisi hatukwenda ki serious kwa sababu raisi amegundua kwamba hii vita haina faida yoyote kwetu. Sana sana tunaweza kupata hasara zaidi kuliko faida.
Hii ni kwa sababu mfadhili mkubwa anaewafadhili hawa M23 ndio mtu wa kwanza au wa pili kupitisha mizigo yake katika bandari yetu na ardhi yetu. Analipa mabilioni ya ushuru kila siku au kila week.
Hivyo tukiingia kwenye vita na mtu huyu ni sawa sawa na kuukata mkono wako mwenyewe unaokulisha. Kumbuka kwamba mfadhili huyo ana ukaribu na amiri jeshi mkuu wetu haswa kuhusu maswala ya kibiashara , upitishaji wa mizigo na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi yetu na nchi ya mfadhili. Sasa tukiwa serious kumtwanga itabidi atukimbie na kwenda kushirikiana na nchi nyingine kama vile Kenya nk.
Hizo ndio sababu kuu za sisi kutoiadhibu M23 kama kipindi kile. Serikali inaangalia hasara na faida inayopata kupitia vita hivi. Tukiwachapa basi hasara itakuwa kubwa kuliko faida. Lakini kwa vile sisi ni sehemu ya SADC na tumechaguliwa kwenda Congo. Basi acha jeshi letu litulie kule kujilia watoto wa kinyamulenge hadi muda ukapofika kurudishwa nyumban waruri kuendelea na maisha. But ukweli utabaki pale pale kwamba hapa East Africa hakuna jeshi wala kikundi cha wahuni kama hicho cha M23 ambacho kitaweza kupambana na JWTZ.