Zijue tabia 4 zinazopunguza kinga za mwili bila kujijua

Feld Marshal Tantawi

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2014
Posts
655
Reaction score
1,069
Kinga ya mwili ni ile hali ya mwili kuwa na uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi mbalimbali.

Mtu anapokuwa na kinga imara za mwili, huepuka kuugua mara kwa mara na kwa kifupi unaweza kusema kwamba kinga ya mwili ndiyo kila kitu katika afya ya binadamu.

Kuumwa mara kwa mara ni dalili tosha kuwa kinga yako ya mwili imeshuka na hivyo unahitaji kuchukua hatua za kuziimarisha.

Kwa kawaida Mungu alituumba miili yetu ikiwa na uwezo wa kujikinga na magonjwa yote, laikini mwili utaweza kufanya hivyo endapo tu utapatiwa vyakula vinavyohitaji ili kuimarisha kinga zake.

Leo tuangalia aina ya vyakula vya kuepuka ili kuzifanya kinga za mwili kufanya kazi zake vizuri.

1. Mhusika anapaswa kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi
Sukari siyo nzuri kwa afya yetu hasa inapotumiwa kupita kiwango. Kiwango cha kawaida cha sukari kinachoruhusiwa kutumiwa ni kijiko kimoja kidogo (teaspoon), kinapozidi hapo huwa kinachangia kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili. Inaelezwa kuwa chupa moja ya soda ina karibu vijiko 6 vya sukari. Hivyo kama wewe ni mnywaji mkubwa wa soda na vinywaji vingine vya aina hiyo, utaona ni kiasi gani unachangia kuharibu kinga zako za mwili.

2. Epuka unywaji wa vileo
Unywaji wa pombe kupita kiasi ni sumu ndani ya miili yetu. hivyo si nzuri pia kwani huweza kuchangia kudhoofisha kinga za mwili.

3. Epuka matumizi ya vyakula vya kukaanga
Vyakula vya kukaanga kama vile chips na vinginevyo, pamoja na vyakula vya kuoka huwa na mafuta mabaya ambayo huwa na tabia ya kutengeneza magonjwa mwilini (fee radicals) ambayo huathiri mfumo wa kinga ya mwili pamoja na chembechembe za nasaba (DNA). Vyakula hivi vinapaswa kuliwa kwa nadra sana au kuepukwa kabisa ikiwezekana.

4. Epuka vyakula vya viwandani (vyakula vya makopo)
Epuka ulaji wa vyakula vya kwenye makopo na badala yake pendelea kula vyakula halisi‘fresh’ na vya asili. Ulaji wa vyakula vya asili, hasa vyakula vitokanavyo na nafaka zisizokobolewa, huwa na idadi kubwa ya vitamini, madini na kamba-lishe ambazo ni muhimu sana katika kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili.
 
Shukrani sana ila hapo kwenye vyakula vya kukaanga sasa sijui tutakula nini? Chapati,Vitumbua Maandazi ,Mchuzi ,Samaki ,Nyama etc vyote ni va kukaanga sasa mbadala wake ni nini?

Je, tutakula Mihogo ,Viazi vya kuchemsha kila siku? Cha msingi i kuzingatia Balance Diet tu.
 
Kinga ya mwili ni ile hali ya mwili kuwa na uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi mbalimbali.

Mtu anapokuwa na kinga imara za mwili, huepuka kuugua mara kwa mara na kwa kifupi unaweza kusema kwamba kinga ya mwili ndiyo kila kitu katika afya ya binadamu.

Kuumwa mara kwa mara ni dalili tosha kuwa kinga yako ya mwili imeshuka na hivyo unahitaji kuchukua hatua za kuziimarisha.

Kwa kawaida Mungu alituumba miili yetu ikiwa na uwezo wa kujikinga na magonjwa yote, laikini mwili utaweza kufanya hivyo endapo tu utapatiwa vyakula vinavyohitaji ili kuimarisha kinga zake.

Leo tuangalia aina ya vyakula vya kuepuka ili kuzifanya kinga za mwili kufanya kazi zake vizuri.

1. Mhusika anapaswa kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi
Sukari siyo nzuri kwa afya yetu hasa inapotumiwa kupita kiwango. Kiwango cha kawaida cha sukari kinachoruhusiwa kutumiwa ni kijiko kimoja kidogo (teaspoon), kinapozidi hapo huwa kinachangia kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili. Inaelezwa kuwa chupa moja ya soda ina karibu vijiko 6 vya sukari. Hivyo kama wewe ni mnywaji mkubwa wa soda na vinywaji vingine vya aina hiyo, utaona ni kiasi gani unachangia kuharibu kinga zako za mwili.

2. Epuka unywaji wa vileo
Unywaji wa pombe kupita kiasi ni sumu ndani ya miili yetu. hivyo si nzuri pia kwani huweza kuchangia kudhoofisha kinga za mwili.

3. Epuka matumizi ya vyakula vya kukaanga
Vyakula vya kukaanga kama vile chips na vinginevyo, pamoja na vyakula vya kuoka huwa na mafuta mabaya ambayo huwa na tabia ya kutengeneza magonjwa mwilini (fee radicals) ambayo huathiri mfumo wa kinga ya mwili pamoja na chembechembe za nasaba (DNA). Vyakula hivi vinapaswa kuliwa kwa nadra sana au kuepukwa kabisa ikiwezekana.

4. Epuka vyakula vya viwandani (vyakula vya makopo)
Epuka ulaji wa vyakula vya kwenye makopo na badala yake pendelea kula vyakula halisi‘fresh’ na vya asili. Ulaji wa vyakula vya asili, hasa vyakula vitokanavyo na nafaka zisizokobolewa, huwa na idadi kubwa ya vitamini, madini na kamba-lishe ambazo ni muhimu sana katika kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili.
Umesikika mkuu ila kwa vyakula vya kukaanga apo panahitaji neema ya Mungu.
 
Nilibahatika kuhudhuria maonyesho ya sadcc yaliyopita ,nilipopitia kwenye banda la taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ,walinipa kipeperushi ambacho kilikuwa kinaelekeza kuhusu vyakula vinavyotakiwa kuepukwa ili usipate ugonjwa wa moyo vitafunio kama mandazi chapati na vitumbua vilikuwemo katika list.
 
Hiyo list mbona ndiyo vyakula vyenyewe vya kila siku.Tungeambiwa na jinsi ya ku neutralize baada ya kula hiyo vitumbua.maandazi chapati nk.

vinginevyo tutajichanganya.kuna watu wanafanya kazi za kutumia nguvu .Je na wao pia wale mboga mboga tuu.nadhani inahitaji elimu pana isiyoangalia ugonjwa wa moyo tu ila mahitaji ya mwili kwa ujumla.

Kwa mfano nikimsikilizaga prof.Jananaba wa taasis ya moyo kuhusu vyakula halafu nikiwa sikiliza taasis ya lishe Tanzania nachanganyikiwaga.

The Botom line.suala la Lishe tuiachie taasis husika inayoshughulikia lishe.

Ijapokuwa hiyo taasisi ya CHAKULA NA LISHE Ya Tanzania haijafanya vya kutosha kutoa elimu. iko kimya sana kama vileTaasis ya usalama wa Taifa.
 
Maandazi , chapati, vitumbua ni vyakula vilivyoletwa na Waarabu na Wahindi. Sisi vitafunwa vyetu ni viazi, mihogo, majimbi ect.
 
Nilibahatika kuhudhuria maonyesho ya sadcc yaliyopita ,nilipopitia kwenye banda la taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ,walinipa kipeperushi ambacho kilikuwa kinaelekeza kuhusu vyakula vinavyotakiwa kuepukwa ili usipate ugonjwa wa moyo vitafunio kama mandazi chapati na vitumbua vilikuwemo katika list.
Hatar mno na ndivo tulivozoea
 
Hiyo list mbona ndiyo vyakula vyenyewe vya kila siku.Tungeambiwa na jinsi ya ku neutralize baada ya kula hiyo vitumbua.maandazi chapati nk.

vinginevyo tutajichanganya.kuna watu wanafanya kazi za kutumia nguvu .Je na wao pia wale mboga mboga tuu.nadhani inahitaji elimu pana isiyoangalia ugonjwa wa moyo tu ila mahitaji ya mwili kwa ujumla.

Kwa mfano nikimsikilizaga prof.Jananaba wa taasis ya moyo kuhusu vyakula halafu nikiwa sikiliza taasis ya lishe Tanzania nachanganyikiwaga.

The Botom line.suala la Lishe tuiachie taasis husika inayoshughulikia lishe.

Ijapokuwa hiyo taasisi ya CHAKULA NA LISHE Ya Tanzania haijafanya vya kutosha kutoa elimu. iko kimya sana kama vileTaasis ya usalama wa Taifa.
Yah bado kuna shida kubwa
 
Back
Top Bottom