Utaratibu wa kufunga ndoa yenu bomani mnatakiwa muwe na barua ya serikali ya mtaa kwaajili ya kuwatambulisha mnapotoka.
Pia mnatakiwa mlipie ada ya kufungishwa ndoa ya shilingi 50,000/-.
Baada ya kuandikisha, mtasubiria itangazwe kwa muda wa siku 21, na baada ya hapo mtafungishwa ndoa.
Na bomani ndoa inafungwa siku ya jumatatu mpaka ijumaa, mkitaka kufungishwa ndoa siku ya jumamosi au jumapili basi mtalipia shilingi 150,000/-.
Na pia mkitaka kufungishwa ndoa nje na ofisi za serikali yaani pale bomani inawezekana ila mtalipia shilingi 300,000/- , na hayo malipo ni mbali na ile ada ya shilingi 50,000/-.
Kwa kufanya hivyo ndoa yako itakuwa imekamilika na kutambuliwa na jamii na mbinguni pia sasa na neno kwenye kitabu cha Rum 13:1-2 imeandikwa, kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu , kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa MUNGU, na ile iliyopo imeamliwa na MUNGU.
Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la MUNGU, nao washindanao watajipatia hukumu.