Cute_Emmy
Member
- Mar 12, 2021
- 17
- 8
Zifuatazo ni tovuti bora ambazo zitakuwezesha kusoma tovuti bure au kwa gharama
1. Jamiiforums
Tembelea tovuti ya Jamiiforums kisha nenda katika jukwaa la Sports & Entertainment halafu chagua jukwaa la Entertainment
Katika jukwaa hili utaweza kusoma simulizi na chombezo mbalimbali bure.
Entertainment
FAIDA
1. Simulizi na chombezo nyingi hutolewa bure, hivyo utasoma bila gharama
2. Utaweza kusoma simulizi kuanzia mwanzo hadi mwisho kama simulizi zilitumwa miezi iliyopita au mwaka uliopita.
3. Utaweza kuweka maoni yako endapo simulizi inapokuwa inarushwa au baada ya kumalizika.
4. Utakutanishwa na watunzi mahiri wa simulizi na chombezo.
5. Utapewa nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa endapo kuna sehemu hujaelewa.
HASARA
1. Sio simulizi na chombezo zote zinafika mwisho, wapo baadhi ya watunzi na watuma simulizi wanaoshindwa kumaliza simulizi (arosto)
2. Kuna baadhi ya simulizi na chombezo zitaishia kati na kukutaka ulipie kiasi flani cha pesa ili uendelee kusoma.
3. Kuna baadhi ya waandishi hufuta "sehemu" za simulizi wanazozirusha, hivyo kupelekea simulizi kukosa mtiririko mzuri.
4. Matumizi mabaya ya lugha kwa wachingiaji , ambapo hupelekea uzi kufutwa.