Zikiwa zimesalia siku 4 TCRA wanena

Zikiwa zimesalia siku 4 TCRA wanena

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Zikiwa zimebaki siku nne laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kufungiwa, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaagiza Watanzania waliokamilisha usajili wa laini zao kuhakiki upya kwa kupiga namba *106#.

“Kama mnavyofahamu, mwisho wa kutumika kwa laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa kutumia namba ya kitambulisho cha taifa (Nida) na kuthibitishwa kwa alama za vidole ni Januari,20, 2020, kama umeshasajili hakiki tena usajili wa laini zako kwa kupiga namba *106# na uchukue hatua stahiki sasa,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa rasmi leo January 16, 2020 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba kwa watu wote ambao bado hawajasajili laini zao za simu na kuwataka kutumia siku hizi nne zilizobaki kukamilisha usajili huo ili kuepuka adha itakayojitokeza mara baada ya laini kufungwa.

Pia amesema zoezi la usajili wa simu litakuwa endelevu hata kwa wale ambao watakuwa wamefungiwa wataweza kufungua laini zao kwa kuzisajili, lakini pia kwa wale ambao watanunua laini mpya pia wataweza kusajili laini hizo.

“Kwa watakaositishiwa huduma za laini zao za simu Januari 20 wanaweza pia kuendelea na utaratibu wa usajili kwa lengo la ama kurudisha laini zao zitakazokuwa zimefungwa au kupata laini mpya. Kwa watumiaji/waombaji wapya wa laini za simu wataendelea kusajiliwa muda wote na usajili huo kwa kutumia kitambulisho cha taifa na kuhakikiwa kwa alama za vidole".
 
TCRA nyie Ni verified users hapa JF, nashangaa mko kimya, taarifa yenu inayahusu Hadi mabasi ya mwendokasi.
Wekeni hapa official statement
Tuna kazi nyingi sana,tukipata mda tutaliongelea hili
 
Hahaa wameona waliofanikisha usajili huo hawafiki hata 10%
Hvyo wanaogopa kupoteza mapato, kama wana nia kweli wazifunge hyo tar. 20 waone watavyopoteza mapato
 
Hahaa wameona waliofanikisha usajili huo hawafiki hata 10%
Hvyo wanaogopa kupoteza mapato, kama wana nia kweli wazifunge hyo tar. 20 waone watavyopoteza mapato
Nahisi wanaweza kufunga kwa siku kama 3 hivi ili kupima upepo halafu baada ya hapo Jiwe ataibuka na yale matamko yake ya kilofa
 
Fungeni tu haina shida,Branch,M-pawa na Songesha sijui mtanipata wapi na line yangu mmefunga wenyewe.Nipo hapa nawacheki kwa dharau na kitambukisho ninacho.Siku hizi mtu akitaka kunitumia ela nampa namba ya wakala anatoa huko huko mi nachukua ela dirishani tu.Na mkifunga sirudishi hiyo line tena....[emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi ni mmoja kati ya wanaoamini kuwa line hazifungwi na kwa kuonyesha msisitizo sijasajili kwa vidole na wala sina mpango.
 
Fungeni tu haina shida,Branch,M-pawa na Songesha sijui mtanipata wapi na line yangu mmefunga wenyewe.Nipo hapa nawacheki kwa dharau na kitambukisho ninacho.Siku hizi mtu akitaka kunitumia ela nampa namba ya wakala anatoa huko huko mi nachukua ela dirishani tu.Na mkifunga sirudishi hiyo line tena....[emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom