Jelavic
Senior Member
- Dec 28, 2016
- 183
- 380
Tukirudi nyuma kidogo,
Tareh 22/6/2022 urusi na Ukraine kwa usimamizi wa uturuki na umoja wa mataifa waliingia mkataba wa makubaliano ambao urusi iliridhia nafaka za Ukraine ziruhusiwe kutoka Ukraine kupitia bahari nyeusi kwaajili program ya umoja wa mataifa ya kuhami nchi masikini dhidi ya balaa la njaa ambalo linaongezeka kwa kasi hasa kwa nchi za afrika ,mbali na mambo mengine mkataba huo ulitokana na shinikizo kubwa la nchi za afrika ambazo ndio zimeathiriwa zaid na vita kiuchumi wakati ambao urusi inatafuta kuungwa mkono zaidi na nchi mbali mbali.
Katika kikao cha 77 cha umoja wa mataifa kilichofanyika wiki iliyopita, Rais Erdoğan wa uturuki aliuita mkataba wa instanbul 2022 kama ni mkataba ulioiokoa dunia dhidi ya janga la njaa.
Hata hivyo tareh 7 mwez wa 9 mwaka huu Rais putin alidai kuwa katika Meli 87 zikizobeba nafaka toka Ukraine ni meli 2 tu kati ya hizo ndio zilibeba nafaka kwaajili ya programu ya nchi masikini , aliendelea kudai kuwa meli hizo mbili zilibeba tani elfu sitini tu katika ya tani milioni 2 ambazo zilitoka Ukraine , huku akidai nafaka zote zilizobaki zilienda nchi za ulaya badala ya nchi masikini.
Inadaiwa ulaya inajiandaa na kipindi cha shitaa, kipindi ambacho kinakaidiriwa kuwa kigumu zaidi kutokana na bei ya nishati kuwa juu pamoja ukosefu wa chakula cha kutosha kutokana na vita inayo endelea kati ya urusi na Ukraine ukijumlisha na athari ya korona ambayo bado ilikuwa haijamalizika
Kwa mujibu wa vyanzo nilivyo navyo, ni meli moja tu ndio iliripotiwa ikielekea nchi za sub-sahara, ambayo ilionekana katika bandari ya djibout,meli ambayo ilibeba tani elfu 23 ambazo ni kwaajili Somalia na Ethiopia kiwango ambacho kitaweza kunufaisha kaya masikini 1.5 milion kwa kipindi cha mwezi mmoja tu.
Wiki iliyopita Rais putin alihoji ziko wapi nafaka mlizodai ni kwaajili ya nchi masikini..?
Kwa mujibu wa Rais putin atakaa tena na Rais wa uturuki ili uangalie upya mkataba huo sabab anadai katika utekelezaji wake haufikii malengo walio kubaliana, Mbali na mkataba huo wa nafaka urusi na Ukraine wameingia mkataba mwingine wa kubadilisha mateka ,jambo ambalo linaashiria mwanzo mzuri wa uwezekano wa kumaliza vita kwa mazungumzo.
30/sep/2022