MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Wasalaam wana JF
Nilipokua mdogo niliambiwa kua uyaone. Nimekua sasa, hakika ya ulimwengu na malimwengu ni mengi na ya kustaajabisha.
katika kipindi fulani niliaminishwa kwamba kuwa mnyonge ndiyo alama ya uzalendo na kwamba asiye utaka unyonge ni kibaraka wa mabeberu au ni beberu kuu lenyewe.
Vita ikatangazwa ya kiuchumi kati ya wanyonge na mabeberu. Ila muasisi wa vita hiyo alipendwa zaidi na muumba. Aidha, ni vigumu sasa kuamua ni nani kati ya wanyonge na mabeberu aliyeshinda.
Kimsingi, kuna mgongano wa fikra kati ya mnyonge na beberu. Beberu anataka kuishi vizuri wakati mnyonge kashindwa kuishi vizuri na anataka beberu aishi kama shetani.
Falsafa ya utetezi wa wanyonge imejengwa katika kutengeneza wanyonge wengi zaidi, na hivyo, ndiyo inayopigiwa makofi na kundi kubwa la watu wasiofikiri vizuri.
Mungu wetu ni mwema, ametuamulia kesi, wamebaki watetezi uchwara wa hao wanaojitabainisha kama wanyonge.
Mwenye kuelewa na aelewe.