Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,484
- 4,826
- Thread starter
-
- #21
Mimi bana sikinde tuuu, jamani sikinde watani wangu msondo mtaniwia radhi. Dah kuna vibao nikivisikia mpaka natokwa na jasho kuna kitu km Duniani Kuna mambo, wikiendi nalala kwa taabu, kwa ujumla sikinde you rock my heart!! ningekuwa na pesa ninge invest trillions pale basi tu sina kitu. haya kuna hawa marques du zaire enzi za kamanyola bila jasho kuna kibao kama dola mtoto wa Dodoma( yakaa yaka eeehn mwana mama ndimandimaeee mwana mama ...... mtoto wa dodoma) kuna kinanda flani kinapigwa mle na gitaa yaani ni raha tupu!! inanikumbusha sana dada yangu marehemu Mage jamani wakati niko Sumbawanga alikuja toka Dar basi anaziimba hizi nyimbo za makwizzz aaah jamani KAMANYOLA BILA JASHO! ikaja telemuka telemuka chekechaaaaaa
Mi mdau sana wa nyimbo za bendi ulizotaja. Swali langu kwako ni umewakumbuka vp wanamziki wote hao? Naomba uanachama kwenye maktaba yako.Pia kuna Orch. Marquiz Original,kundi hili liliundwa miaka ya 70 na wanamuziki waliotoka katika jimbo la Shaba nchini Zaire(DRC) waliingia nchini wakiitwa Orchestre Super Gabby,baada ya kuingia nchini walibadilisha jina na kuanza kuitwa Orchestra Maquis du Zaire/Marquis Original.....Mitindo waliyoitumia ni pamoja na Ogelea Piga Mbizi,Zembwela na Sendema.....Ukumbi waliokuwa wakipiga(uwanja wao wa nyumbani) ni Lang'ata Social Hall pale Kinondoni(FM Club ambapo kwa sasa ni kanisa).....Hawa pia walikuwa wanaujua muziki hasa kutokana na aina ya muziki mchanganyiko wa kizaire(kavasha) na vionjo vya kitanzania walivyopiga....Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana,nyimbo kama Mayanga,Ngalula,Makumbele,Mpenzi Luta,Mpenzi Scola,Karubandika,Seya,Tipwatipwa,Kisabengo,Wakati nilikuwa mdogo,Bi Sofia,Hali ngumu,Ni wewe pekee,Kibulwa,Huba wangu,Mapenzi sio masihara,Wanaume wa leo,Clara,Mayasa,Wema wangu,Double double,Mabruki,Anjelu,Balimwacha,Kazi yangu Baharia,Mapenzi ya pesa na nyingnie nyingi....Hawa jamaa wanaweza kuwa wanaongoza Tanzania kwa kuwa na nyimbo nyingi sana....Bendi hii imewahi kuwa na wanamuziki kama Tshimanga Kalala Assosa,Issa Nundu,Mukumbule Lulembo 'Parash',Mbuya Makonga 'Adios',Ilunga Banza Mchafu.Dekula Kahanga 'Vumbi',Bobo Sukari,Fredito Butamu,Mbwana Kocks,Kabea Badu,Mutombo Lufungula Audax,Matei Joseph,Kaumba Kalemba,Mukuna Roy,Berry Kankonde,William Maselenge,Seif Said,Nguza Vicking,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Kiniki Kieto na wengine kibao..............Hakika ya kale ni dhahabu...
Hahaaaaaaaaa,nimekusoma Home boy,nitafanya utaratibu wa kukutumia,shaka ondoa Nkwingwa...
bwana mzee unanikumbusha mbali sana,lakini ndio hivyo miziki inakufa sijui nani aje aokoe hili
kila siku nafikiria nitoe mchango gani bendi hizi zirudi lakini nashindwa
nakuuliza kaswali kadago,reheni bichuka yuko hai?je yuko wapi na maisha yake yakoje?
Si wewe tu mkuu wangu,kila mtu akizikumbuka bendi kama Marquis(wana sendema,zembwela n.k),Sambulumaa,Vijana Jazz(pambamoto),Washirika Tanzania Stars(watunjatanjata,njata one),Tancut Almas(wana fimbo lugoda,kinyekinye kisonzo tisa kumi mangala),JKT Mafinga(kimulimuli),JKT Kimbunga stereo,Ngorongoro Heroes Band(sukuma push),Kurugenzi Jazz,Six Manyara,Bima Lee(Magnet tingisha),Super Matimila(Bongo beats,talakaka),Zaita Musica(wana zuke muselebende),MK Group(wana Ngulupa tupatupa dansi),MK Beats(wana tukunyema,wowowo),MK Sound,OSS(wana masantula ngoma mpwita,dukuduku,ndekule,power Iranda,rashikanda wasaa),MCA Internationa(wana munisandesal,Orch. Makassy,Magereza Jazz(Mkote Ngoma),Bicco Stars(wana kindumbwe ndumbwe),Super Rainbow,Bantu Group Band(wana kasimbagu kaabuka),Legho Stars(wana sopabango),Afriso International ya Lovy Longomba na nyingine nyingi.......Nyingi kati ya bendi hizi zimekufa na zilizopo zinajikongoja........Natamani kuurudisha wakati nyuma aisee....
Kuhusu Super Stereo Hassan Rehani Bitchuka,kwa sasa yupo Mlimani Park orch wana Sikinde ambako alihamia akitokea Msondo Ngoma....
Mkuu uko juu...
Mimi nakumbuka Orchestra Makassy chini ya Mzee Kitenzogu "Mzee" Makassy...enzi hizo akiwa na marehemu Dr Remmy Ongala kabla hajaanzisha Matimila...
Mi mdau sana wa nyimbo za bendi ulizotaja. Swali langu kwako ni umewakumbuka vp wanamziki wote hao? Naomba uanachama kwenye maktaba yako.
Bala, huwakumbuki Mzinga Troupe ya Moro? Waliibuka na kibao kiitwacho mazoea yanikondesha kilichotungwa na kuimbwa na Issa Mrisho kwa sauti nzuri sana. Kibao hicho kikipigwa hata leo utadhani ni cha jana. Baadhi ya Masahiri ni haya
Mazoea yananikondesha eee
Sio kama nimelishwa kizizi, labda,
Laini siamini alijua matatizo
Hata Mjusi hata Kinyonga,
wao hula Vijidudu hai
Hasa vyenye kurukaruka, mbona yeye hana mbawaaaa
Anapata riziki yakeee, sembuse mimi mwanadamu
Bala, umtaja Kurugenzi Jazz, bila shaka ni ile ya Arusha iliyokuwa na kibao kikali sana Wivu
Wivu ukizidi nyumbani mapenzi yapunguaa
Wivu usiyo na maana waleta hasara
Umefanya kitu gani, bibi umemkataza kufanya kazi
ati sababu wachelelewa nyumbani....
Kibwagizo
Maisha ya leo, ni kufanya kazi
Mke na mume, kusaidiana
Mkuu Balantanda big up sanaaa!!
Tusisahau pia UDA Jazz wana Bayankata...kama sikosei Ally Choky alianzia huko
unanikumbusha MOLEMA na siku ya kufa alioimba DR. REMMY wakati akiwa makassy. kuna mosese hawa jamaa nao waliimba bana. jf kulikuwa ns zilipendwa MODS kwa nini mmeziondoa jamani?Mkuu uko juu...Mimi nakumbuka Orchestra Makassy chini ya Mzee Kitenzogu "Mzee" Makassy...enzi hizo akiwa na marehemu Dr Remmy Ongala kabla hajaanzisha Matimila...
kWANINI SAFU YA WAIMBAJI KARIBU WOTE WALOTAJWA HAPO JUU 'WAMENUNA' WAMEFARIKI DUNIA?Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....
Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.......
Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba,Hekaheka,Heka koka,Watoto wa nyumbani,Air Pambamoto(awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.....
Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa......Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku,Mary Maria,Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto,Adza(Aza),Ngapulila,Ogopa Tapeli,Mwisho wa Mwezi,Penzi haligawanyiki,Wivu,Malaine,Nyongise,Shoga,Theresa,V.I.P,Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu....
Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku',Hamza Kalala 'Komando',Manitu Mussa,Issa Chikupele,Hassan Dalali,Hassan Shaw,Ally Jamwaka,Abuu Semhando,Bakari 'Baker' Semhando,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya zege',Eddy Sheggy,Shaban Yohana 'Wanted',Rashid Pembe 'Profesa',Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo,John Kitime,Abdallah Mgonahazelu,Freddy Benjamin,Mohammed Gotagota,Said Hamis 'Misukosuko',Athumani Momba na wengine kibao...
Haaa Bala umeturudisha kwenye mambo yetu yaleeeee,
Vijana walikuwa machachari na ndio walikuwa bendi neutral ya wapinzani wa Jadi DDC na Msondo
Umenikumbusha Dudumizi mtaalamu wa nyimbo za mapenzi[/QUOTE
Jamaa(Jerry Nashon Dudumizi) alikuwa mtunzi kwelikweli wa nyimbo za mapenzi hasa akiwa na Bima Lee na Vijana Jazz...
Angalia kama kitu hiki kitamu hapa chini ambacho ni utunzi wake..
V.I.P-Jerry Nashon 'Dudumizi"
(Wote): Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo,
(Dudumizi): Si maji wala Soda vitakavyozima kiu yangu,ila ni wewe VIP,
Si maji wala Soda vitakavyozima kiu yanguuu,iila ni weweeeee,VIP
Baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa,na kisirani cha kufokewa na boss,
Nahitaji VIP wa kunibembeleza,nakutaka wewe mama,unibembeleze,
Si kwa maneno ila kunitomasatomasa,kwa mikono yako laini yenye bangili,
Unipe busu mwanana la kunipumbaza wee (VIP).
Baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa,na kisirani cha kufokewa na boss,
Nahitaji VIP wa kunibembeleza,nakutaka wewe mama,unibembeleze,
Si kwa maneno ila kunitomasatomasa,kwa mikono yako laini yenye bangili,
Unipe busu mwanana la kunipumbaza wee (VIP)
(Wote): Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo,
Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo.
Dudumizi: VIP sogea karibu,ubipe busu mwanana mama
(Wote): Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo,
Bridge
(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.
Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka
Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP,
Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP
Natamani penzi live sio penzi la ndotoni,nakuomba uwe wangu VIP,
Tafadhali nakusihi, ili niondokane na ndoto za mapenzi.
(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.
Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka
Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP,
Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP
Natamani penzi live sio penzi la ndotoni,nakuomba uwe wangu VIP,
Tafadhali nakusihi, maaa mamaa,maaa....maaa yoooo,maa mamamaaaaaaaaaaaaaaa,
Tafadhali nakusihi, ili niondokane na ndoto za mapenzi.
Dudumizi: Ukinikubali VIP,mimi niko tayari,kubadili dini,
Ukinikubaliii VIP mimi niko tayari,kubadili dini,
Hata kama wazazi wangu hawapendi,nitafanyafanya mipango niwe na wewe sambamba(sambamba)
nitafanyafanya mipango niwe nawee sambambaaa
(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.
Ukinikubalii VIP,mimi niko tayari kubadili dini,
Ukinikubalii VIP,nitatoa mahaliii ya mbuzi saba,
Hata kama sina VIP,nitafanyafanya mipango niwe na wewe sambamba(sambamba) nitafanyafanya mipango niwe na wewe
sambamba.
(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.
:music::violin::music: