ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Balantanda tafadhali huu wimbo uliitwaje?
Bado na asili navyo na kamwe sitobadilika
Japo kuwa unajitamba na cheo kujiongezea
Bure utakonda na mwili kukupooza
Umejiingiza katika mambo
Mambo ya siyo kuhusu
Mwiba huchoma kote kote
Si rahisi kukosa
Wewe bado bwana mdogo hata chini hujakaa
 
Kuna mwingine unasema "wengi wamelazwa hospitalini na kuwekewa P.O.P shauri yako Hawae,Hawae P.O.P aah P.O.P......"
Nani anakumbuka umepigwa na nani?
 
Habarini, leo nimepanda daladala nikasikia nyimbo mbili za bendi fulani za zamani, nilikuwa dogo ila nilikuwa najitambua! Nimeusikia wimbo huu nimekumbuka mbali sana tabora, nimeshawishika nitafute hizi nyimbo na zingine za kina hamza kalala komando ila sijui pa kuzipata.
Nimesikia hizi nyimbo mbili chini ktk daladala ila sizijui majina wala walioimba nikajikuta nimesafirishwa mpaka miaka ya 90s.
-Bwana mwangusi nakupa pole sana watu hao ni walaghai wanaitwa matapeli......

Mwingine huu;

-hunijali kwa chumvi hunijali kwa sukari tabu nyingi ninapata na watoto......

-Vijana wengi hukosa adabu iieee wakishajua huyo si mama yake ieeee humdharau na kumsimanga iiieeeee.......

Old is gold!!
 
Hizi nyimbo zinapatikanaje?
 


Hiyo bwana mangushi ni Ogopa matapeli ilipigwa na hao Vijana Jazz, ninayo kwenye Kompyuta yangu online nimeicheki sikuipata.
 
Kuna mwingine unasema "wengi wamelazwa hospitalini na kuwekewa P.O.P shauri yako Hawae,Hawae P.O.P aah P.O.P......"
Nani anakumbuka umepigwa na nani?
cc Balantanda anaweza kutusaidia kupata huu wimbo wa MINUO YA MAQUIS DU ZAIRE ORIGINAL mkuu naomba msaada wako Kwa hisani yako kiuungwana tu
 
Amani Iwe nanyi wakuu,
Baada ya Kuteseka na Kuhangaika huku na kule mitandaoni nikitafuta ni wapi nitapata Ku-download ngoma zote za hapo kitambo na kukosa, basi nimeona nifungue Blog yangu ZILIPENDWA ambapo kila muda naweka Nyimbo mbali mbali zilizowahi kuwika hapa Barani Africa. Nyumbani ndio kwa Sana.
Hivyo basi wale wadau wote wa Muziki wa Kale Tukutane >>> HAPA <<<
Wadau wote wa KILWA JAZZ, MSONDO, JUWATA, SUPER RAINBOW, TABORA JAZZ, SUPER MATEMBELE, IN AFRICA, MASHROOM, LESS WANYIK/SIMBA WA NYIKA nk BOFYA >>> HAPA twende Pamoja.

Shukran.
 
Safi sana ushauri toa e mail au namba za simu ili wadau waweze kutumia nyimbo nyingine ambazo wanazo kwa kupitia whatsapp au e mail
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…