|
| Majaliwa aipa Sikinde Fadhili ya Punda na Ruhazi Ruhazi |
...Kwa kuongezea kulikuwa na mtu anaitwa Ally Makunguru alikuwa akipiga 2nd Solo na some times rythm gitaa na mpiga drums anaitwa Chipembele Saidi. Kwa ambao kazi yake hawaifahamu vizuri kuna wimbo unaitwa Kata ya maji ukweni..jamaa amekaanga vyepe humo sio pole pole.Pia kulikuwa na bendi ya Orchestra Safari Sound ambao baadaye walikuja(mwaka 1985) kuitwa International Safari Sound,hawa ni wakali wengine waliotamba sana katika muziki wa Dansi wa Tanzania katika hiyo miaka ya 80 na 90...Bendi hii ilikuwa ikimilikiwa na mfanyabiashara Hugo Kisima.....Bendi hii ilikuwa mara nyingi ikifanya maonesho yake katika ukumbi wa Safari Resort uliopo Kimara.....Bendi hii ilitumia mitinfo ya Dukuduku,Ndekule,Rashikanda wasaa na Power Iranda...
Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana kama ilvyo kwa Orch. Marquiz Original.....Baadhi ya nyimbo zao zilizotamba ni kama Marashi ya Pemba,Mwaipungu,Mwana kwetu,Somboko amba,Siri ya mapenzi,Kipipa Ayubu,Takadiri,Mashaka nakonda,Dunia msongamano,Hasira za chunusi,Christina Moshi,Fordy,Sosy,Homa imenizidia,Majuto,Chatu mkali,Kaka Kinyogoli,Shukrani kwa mjomba,Usicheze na bahari,Marcelina,Mayasa,Matatizo ya ukewenza,Mageuzi na nyingine nyingi.....
Bendi hii iliundwa na wanamuziki kama Freddy Ndala Kasheba(R.I.P),Hassan Rehani Bitchuka,Muhidin Maalim Gurumo,Abel Barthazar,Nguza Vicking,Shaban Dede 'Kamchape,Hassan Shaw,Mhina Panduka,Benno Villa Anthony,Lister Elia,Kassim Rashid,Charles Ngosha,Ally Makunguru na wengine wengi......
Mtafute John Kitime wa wana Njenje yeye ni kama iliyokuwa RTD,wanapiga Salender bridge au mcheki kwenye FBMe niko tayari kutoa kiasi chochote reasonably kupata hizo nyimbo,anyone???yeah,and I may also take for free!!
Nipo wimbo wao moja tu maana ndo ilikuwa yangu hiyoBila kuwasahau Bima Lee Orchestra....Bendi hii ilikuwa ikimilikiwa na Shirika la Bima la Taifa.....Iliimarika zaidi mwaka 1984 baada ya kuwapata wanamuziki kutoka bendi tofauti tofauti walipoletwa kwenye bendi hii kwa lengo la kuiimarisha....Wanamuziki hao ni Shaban Dede,Jerry Nashon 'Dudumizi',Joseph Mulenga,Abdalaah Gama na Athuman Momba....Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa Magnet 84 na baadae uliboreshwa ukawa Magnet ndele Tingisha.....
Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Neema,Shangwe ya harusi,Makulata,Linalonisibu,Milionea wa mapenzi,Linalonisibu,Siri yako,Visa vya mesenja,Uzuri ni tabia,Dunia ni upepo,Busu pande tatu,Ndoa fungo la hiyari,Penzi dawa ya chuki,Samaki baharini,Baba Shani,Shakaza na nyingine nyingi....
Bendi hii iliundwa na wanamuziki kama Shaban Dede,Athuman Momba,Joseph Mulenga,Abel Barthazar,Abdallah Gama,Belesa Kakere,Maxmilillian Bushoke,Jerry Nashon,Coumson Mkomwa,Eddy Sheggy,Fresh Jumbe na wengine wengine
Mkuu wangu sana Ngambo Ngali.....Balantanda, hujawatendea haki Vijana Jazz Band kama hutataja wimbo wa mesenja kazua balaa
Mambo yote tancut almasi orchestra, wana mangala dance-kinye kinye kisonzo. Kalala mbwembwe, john kitime, mapacha kasalo na kyanga songa, kibambe ramadhani, kawelee, father kidevu-abdul salvador. We bwana wacha!
Bil kuvisahau vibao kama Mama,Tutasele, Mbuguswa na Masafa mrefu...
Hivi mnkumbuka kile kibwagizo cha 'akina mama mwipulikeee,ieeee mwipulikeee........Mbuguswaaaa'