leo ndipo nimegundua kuwa kumbe kijiwe hiki kinapiga mziki wa enzi zetu. Kilichoniboa ni kuwa nyimbo nyingi ama zimepewa majina yasiyokuwa sahihi ama zimeonyeshwa kuimbwa/ kupigwa na waimbaji/bendi zisizo sahihi. Ninataka kusahihisha makosa ya aina hii kwa nyimbo zote zilizopigwa mwishoni mwa miaka ya sitini, miaka ya sabini na mwanzoni mwa miaka ya themanini. Je nifanyeje ili kuweka masahihisho hayo?