Zimamoto IIala wadhibiti moto Kariakoo (Julai 4, 2021)

Zimamoto IIala wadhibiti moto Kariakoo (Julai 4, 2021)

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Kariakoo inaungua na moto muda huu

======

Dar es Salaam: 04.07.2021

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, limefanikiwa kudhibiti moto uliokuwa ukiwaka katika nyumba inayomilikiwa na familia ya Mussa Pazi, iliyopo mtaa wa Mafia na Msimbazi, Kariakoo.

Chanzo cha moto huo ambao ulianza kuwaka muda wa saa moja na nusu asubuhi hadi saa nne na nusu hivi, bado hakijafahamika.

Kwa mujibu wa Afisa wa Oparesheni kutoka Jeshi la Zimamoto na uokoaji Wilaya ya Ilala, ABDALLAH ULUTU, amesema baada ya kupokea taarifa za moto huo Walifika mapema ili kuudhibiti.

Amesema moto huo, licha ya kudhibitiwa umeunguza na kuharibu mali mbalimbali zilizokuwepo kwenye milango ya biashara kwenye nyumba hiyo.

"Hadi sasa hakuna vifo wala majeruhi waliotokana na ajali hiyo ya moto," amesema Afisa huyo wa Oparesheni wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji.
 
Kariakoo ipi maana karibu kila Mkoa Tanzania kuna mahali panaitwa Kariakoo! Isije kuwa Katiakoo ya Dodoma.
 
Mbona TBC wanagonga Music badala ya breaking news.. TBC wako kamatia kamata..kamataaaa (in diamond's voice)
 
Back
Top Bottom