Zimamoto kujiimarisha kidigitali

Zimamoto kujiimarisha kidigitali

lwambof07

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
4,643
Reaction score
5,335
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini limesema kwamba litaboresha mifumo yake ya kidigitali katika utoaji wa taarifa kwa umma, utakaowezesha kutoa taarifa kwa wananchi wengi kwa wakati mmoja ili kutatua changamoto za majanga ya moto.

Kauli hiyo imetolewa na Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto Tanzania Puyo Nzalayaimisi, wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari vya makampuni ya IPP Media, ambapo aliongozana na maafisa habari wa jeshi hilo kutoka mikoa mbalimbali ya zimamoto mkoani Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala Elinimo Shang'a, ameeleza matembezi ya jeshi hilo yatakayowahusisha na wamachinga katika uhamasishaji kwa wananchi kutumia namba ya dharura ya jeshi hilo katika kupata usaidizi pindi majanga yanapotokea.

IMG_20220211_094458.jpg
 
Hao the so-called FIRE viazi mbatata hata wangepewa rockets zote za Elon Musk, Russia na China, bado watachelewa eneo la tukio.
 
Wameshindwa kuishauri serikalini kuweka mifumo ya water hydrant maeneo muhimu ya majengo ya umma wataweza Mambo ya digital kweli?[emoji848]
 
Wameshindwa kuishauri serikalini kuweka mifumo ya water hydrant maeneo muhimu ya majengo ya umma wataweza Mambo ya digital kweli?[emoji848]
Naona kwao naona hilo halina umuhimu ndiyo maana wakaamua kuja na ajenda nyingine
 
Duh mbona mnawakatia tamaa hivyo
Mafanikio hakuna. Mioto inajiwakia hadi inazima, ndipo wanakuja, tena bila maji na vifaa muhimu. It's as if mioto kabla ya kulipuka inawapa rushwa maafisa wa zimamoto.

Actually, lile neno la kisasa, ^zimamoto^ (kufanya kazi kwa purukushani, ubabaishaji na kuchelewa, kushughulikia athari badala ya kudhibiti chanzo), ndilo hasa linawahusu hawa jamaa.
 
Back
Top Bottom