Zimamoto: Taarifa za Soko la Karume kuwaka moto hatukuzipata mapema

Zimamoto: Taarifa za Soko la Karume kuwaka moto hatukuzipata mapema

lwambof07

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
4,643
Reaction score
5,335
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Ilala Elisa Mugisha, amesema kwamba taarifa za kuungua kwa soko la Karume walichelewa kuzipata kwani wangezipata mapema wangeweza kuokoa athari iliyojitokeza.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 18, 2022, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, na kusema licha ya kufika na kukuta moto umekua mkubwa lakini pia mazingira ya sokoni hapo si rafiki kwani hakukuwa hata na nafasi ya kupitisha gari.

"Watu waliuona moto mapema, lakini wakaanza kupambana na moto na sisi tumepata taarifa saa 9:12 usiku, tumefika pale saa 9:30, sisi tuko mbali kidogo tunauona moto umeshakuwa ni mkubwa, pale tarifa hazikutolewa mapema," amesema Kamanda Mugisha.

Aidha ameongeza kuwa, "Kulikuwa na magari manne ya kuzima na tulizunguka sana kulingana na mazingira ya pale, taarifa ingetolewa mapema tungeudhibiti, na waliokuwepo walipoona moto umewashinda wakaanza kuokoa mali zao,".

Screenshot_20220118_115140.jpg

Sijaelewa yaani kutoka Faya hadi Karume wametumia dakika zaidi ya 10? Walipitia Kariakoo au walizungukia Magomeni? Tena ikumbukwe ilikuwa saa tisa usiku.
 
Sijaelewa yaani kutoka faya hadi karume wametumia dakika zaidi ya 10? Walipitia kariakoo au walizungukia magomeni? Tena ikumbukwe ilikuwa saa tisa usiku.
Kuna askari kujiandaa na kuandaa vifaa, gari kujaza maji yao yale (bila shaka huwa hayakai na maji muda kwenye matenki yake yale, mnaweza nisahihisha), jumlisha na kusafiri hadi eneo la tukio.
 
Kuna askari kujiandaa na kuandaa vifaa, gari kujaza maji yao yale (bila shaka huwa hayakai na maji muda kwenye matenki yake yale, mnaweza nisahihisha), jumlisha na kusafiri hadi eneo la tukio...
Unaujua utendaji wa zimamoto? Ingia youtube uone, yote unayoyasema hayazidi dakika5
 
Kuna askari kujiandaa na kuandaa vifaa, gari kujaza maji yao yale (bila shaka huwa hayakai na maji muda kwenye matenki yake yale, mnaweza nisahihisha), jumlisha na kusafiri hadi eneo la tukio...
Dakika zote hizo ndiyo maana wanafeli halafu na bado wakienda maji hawana[emoji848][emoji848]
 
Unaujua utendaji wa zimamoto? Ingia youtube uone, yote unayoyasema hayazidi dakika5

Weka link, maana ukiingia youtube channel ya Zimamoto ya Tanzania hakuna video inayoelezea hizo mambo za response time n.k
 
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Ilala Elisa Mugisha, amesema kwamba taarifa za kuungua kwa soko la Karume walichelewa kuzipata kwani wangezipata mapema wangeweza kuokoa athari iliyojitokeza.
Hawa zimamoto ni wajinga sana. Nadhani Kuna haja ya kuiondoa zimamoto kwenye jeshi la polisi maana polisi Wana tabia za kishenzi siku zote.

Ifike wakati zimamoto iwe independent institution chini ya wizara ya mambo ya ndani Yani ksiwe ya kuchukua mapolisi.

Zimamoto ifanye recruitment zake na mafunzo yanayojitegemea na isimamiwe na kiongozi wake asiye polisi.

Polisi no wazembe, wezi, wahuni na wana tabia za kudharau matukio, wakisikia sema wanajivuta sana kwa sababu hakuna rushwa hapo zimamoto.

Ukitaka kupata zimamoto wake haraka mwambie Kamanda kuna hela yako atawakimbiza Kama mbwa.

Zimamoto isimamiwe na polisi Wala polisi asifanye kazi zimamoto sioni kazi yoyote ya kipolisi inayohitajika kwa zimamoto
 
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Ilala Elisa Mugisha, amesema kwamba taarifa za kuungua kwa soko la Karume walichelewa kuzipata kwani wangezipata mapema wangeweza kuokoa athari iliyojitokeza.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 18, 2022, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, na kusema licha ya kufika na kukuta moto umekua mkubwa lakini pia mazingira ya sokoni hapo si rafiki kwani hakukuwa hata na nafasi ya kupitisha gari.

"Watu waliuona moto mapema, lakini wakaanza kupambana na moto na sisi tumepata taarifa saa 9:12 usiku, tumefika pale saa 9:30, sisi tuko mbali kidogo tunauona moto umeshakuwa ni mkubwa, pale tarifa hazikutolewa mapema," amesema Kamanda Mugisha.

Aidha ameongeza kuwa, "Kulikuwa na magari manne ya kuzima na tulizunguka sana kulingana na mazingira ya pale, taarifa ingetolewa mapema tungeudhibiti, na waliokuwepo walipoona moto umewashinda wakaanza kuokoa mali zao,".View attachment 2086168
Wanatuchanganya. Kuna mmoja siku ya tukio alisema walitokea mahali pengine kuzima moto. Na alisema wamewahi ila vifaa duni vikawakwamisha
 
Back
Top Bottom