ZIMBABWE: Tanzania imejifunza nini?

changamoto

Member
Joined
Aug 26, 2008
Posts
11
Reaction score
0

KWA KUWA tuko mbali hatujui kwa hakika maafa yaliyowafika Wazimbabwe katika kipindi cha miaka mifupi tu kutokana na kuwepo kwa chama kimoja kinachodhani kimepewa ahadi na Muumba kutawala milele.


Jamii yoyote inayokipa kikundi chochote katika jamii kuwa na nguvu na uwezo zaidi kuliko makundi mengine katika jamii kinafanya hivyo kwa hasara yake chenyewe.

Nadharia ya 'power' katika jamii inataka mgawanyo wake uwe kwa uwiano mzuri ambao hauruhusu labda wanasiasa wa mrengo fulani kunyanyasa watu wengine au wafanyabiashara fulani kuwa na nguvu za kutisha katika jamii au mangimeza fulani kuibia nchi bila watu wengine kujua kwa sababu tu taifa limeshindwa kuwa na wakaguzi wanaojua ujanja wa wajanja kama wao katika kujinufaisha kutokana na keki ya taifa iliyo meza ya ndani au wachimbaji madini fulani kunywa chote kinachopatikana na kuwaacha wananchi hoi.

Tuiangalia ' theory of power' kwa kuitazama Zimbabwe kwa karibu zaidi na kuona ni hatua gani amabzo sisi kama Watanzania na wazawa wa nchi hii tunaweza kukifanya ili yaliyojitokeza huko yasije yakazuka hapa baada ya miaka michache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…