Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Zimbabwe imerejesha marufuku ya kutotoka nje na karantini za lazima kwa wasafiri wote huku kukiwa na ongezeko la visa vya Covid ili kuzuia kuenea kwa aina mpya ya kirusi cha Omicron.
Nchi hiyo imerekodi zaidi ya visa 130,000 vya Covid na takriban vifo 4,700 tangu janga hilo lianze mapema mwaka jana.
Mamlaka ya Zimbabwe iliimarisha masharti ya Covid-19 ikitaja ukosefu wa uwajibikaji upande wa umma na wanaamini kuwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi msimu wa sikukuu unapokaribia.
Pia kuna hofu ya wimbi la nne.
Rais Emmerson Mnangagwa alipitisha tena amri ya kutotoka nje kutoka saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi saa za huko.
Wasafiri wote wa kimataifa watahitajika kupimwa wanapowasili na kuwekwa karantini katika kituo kilichoteuliwa na serikali kwa gharama zao wenyewe.
Biashara zote zitahitajika kufungwa saa moja usiku.
Masharti hayo ni pigo kwa sekta ya utalii, ambayo ilitarajia msimu wa kawaida wa sikukuu.
Hatua hizo zitatathminiwa baada ya wiki mbili.
BBC Swahili