Zimebaki siku 166 kwenye mwaka

Salaam...

Mpaka kufikia leo tumeshatumia takribani siku 200 kwenye huu mwaka na hivyo kubakiwa na siku 166.

Tujifanyie tathmini ndogo tu, umefanikisha kwa kiasi gani mipango yako ya mwaka huu 2020?

(Rate from 0-10)

Kwangu mpaka sasa ni 3/10
Huu ni mwaka wa ku survive mkuu.

Ukiumaliza unashukuru sana.

Nimeona mpaka nchi zilizoendelea nyingi zimesema zimeondoa malengo ya kiuchumi yaliyowekwa awali.

Mimi nashukuru mpaka sasa nimesimama imara, nachangia jamii kwa kufanya kazi na kutoa misaada kwa waliokwama.

Nahudumia familia yangu.

Naanzisha kituo cha afya sehemu yenye uhitaji.

Najiendeleza kiutashi.

Nimejiwekea mipaka ya mahusiano ya kijamii na nimeiheshimu.

Sijakunywa pombe tangu May 31 2020 na naendelea vizuri katika lengo langu la kupumzika pombe.

Ninaangalia afya yangu ya mwili na akili vizuri.

Nimebarikiwa kurudishiwa hela nilizowapa watu mikopo na kusahau kama watanilipa.

Mwaka si mzuri, annus horribilis. Lakini ungeweza kuwa mbaya zaidi.

Out of ten?

One love.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…