Sidaiani na TCRA.
Utani,
Kiafya: Nimeanza kutoka kitambi, nilianza mazoezi nikaacha baada ya miezi miwili, nimeacha kula kwa mama ntilie na mtaani lazima nirudi home, no sigara, sober for mwaka mzima.
Kielimu/Maarifa: Sijaudhuria ata semina moja, sijasoma ata kitabu kimoja, nimesikiliza podcasts zaidi ya 200hrs, nimeanza Msc, nimesoma course English British council.
Kikazi: Kazi ile ile, inaboa, coworkers walewale, wanaboa, nimeenda shule wamenitolea vihela flani allowance, nalipiwa ada na bodi (HESLB) ila haifanani na allowance nilizokatwa.
Kipato/Mshahara/Maendeleo: Ulele iliongezela elfu 7, Sijajiajiri, Matumizi yameongezeka, sina kiwanja, nimehama ubungo nimeamia Mbagala chamazi,
Mahusiano: Nimegombana na 80% ya ndugu, sina marafiki, nimepiga chini michepuko 98%, naendelea vizuri na girlfriend wangu.
Mengineyo: Nina namba ya NIDA, nimepiga kura, Sina furaha, maisha magumu,
Hitimisho: mwakani siweki goal ata moja nitaenda kibubu bubu tu haya maisha unapanga hivi yanakuja vile.