Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Mojawapo ya methali za Kiswaheli ni hii hapa zimwi likujualo halikuli likakwisha.. Ni methali inayopingana kwa namna fulani na ile isemayo kumkoma nyani giladi hii si ya Kiswahili ni ya kabila la Wandengereko watu wa asili ya Pwani yenye maana ya kwamba ukimuua nyani usimuangalie usoni (maana utamuonea huruma)
Zimwi ni aina ya mnyama mkubwa wa mwituni wa kutosha sana wa enzi za kale.. Ni mnyama wa kufikirika pia
Zimwi ni hayawani kwa maana ya kwamba hana utashi wa kibinadamu na kwamba anaweza kukufanya lolote lile bila sababu yoyote ile ikiwemo kukumeza ama kukukula
Inasemekana hapo kale mababu zetu waliokuwa wanaenda kuwinda wengine walikutana na madhila ya kuuliwa na kuliwa na wanyama wa mwituni yakiwemo mazimwi
Sasa kwenye harakati za mwituni hutokea mwindaji akakutana na zimwi akiwa na windo lake.. Huyu mwindaji asipombughudhi huyu zimwi siku ikitokea bahati mbaya wanakutana tena lakini this time akiwa yeye ndio windo basi zimwi atamla na kumbakisha kichwa kama uthibitisho kwamba haupo tena duniani na ndugu na jamaa zako wapate cha kuzika!
Wanyama wengi sala watu kuacha wale wanaomeza hubakisha kichwa.. Kubakisha kichwa ni alama ya utambuzi.. Kwahiyo wanyama pamoja na uhayawani wao lakini Hufanya hili jambo kubwa sana la kiroho..
Hawabakishi kiungo kingine kama miguu au mikono ni wachache sana hula kila kitu kama wale wa Katavi
Asili ya mwanadamu ni kuzika na uthibitisho wa kifo ni sura kisha mwili.. Japo kuna ambao hufia kwenye majanga mbalimbali na miili yao isipatikane tena.. Hawa huwekewa msiba na taratibu zote za maziko.. Baadhi ya tamaduni huzika mgomba ama nguo za anayehisiwa kafa Na baada ya hapo huanua tanga na kumaliza msiba.. Kama ulipotea tu na ukahisiwa umekufa siku ukionekana watu watakukimbia wakidhani wewe ni mzimu
Pamoja na binadamu kuitwa kiumbe mwenye silika utashi na kustaarabika huku mnyama akiitwa hayawani.. Lakini kuna binadamu ni hayawani kuliko hata hayawani wenyewe
Kama mnyama anaweza kuacha ushahidi wa kichwa kwamba kakuua ili ndugu waweke msiba na waanue tanga kinachomshinda binadamu kufanya hivyo ninini?
www.jamiiforums.com

Sanaa ya kifo
Hii ni habari ngeni kabisa kwa wale watakaobahatika kusoma hii mada na pia wale wenye kupenda kujifunza vitu vipya ni sanaa ya kifo katika uhalisia wetu bila kuchanganya na doctrines za kiimani na kiasili. Kwenye mada nyingi tumeona uhayawani wa mwanadamu tumeona kwa sehemu kubwa jinsi kiumbe...
Ziraili wa gizani
Asili ilipochagua usiku iwe ndio wakati wa kulala kuna siri kubwa ilifichwa huko Kifo kinauma sana hasa anapoondoka mtu tumpendaye sana...nafuu ni kwamba unajua kwamba kafa na hutaweza kumuona tena..... Kuna hili la kupotea watu -kuna watu wanapotea kisha wakaonekana wakiwa hai hata kama wana...