Zimwi linaloila na kuimaliza board ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu???

REAL ACTIVIST

Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
39
Reaction score
5
Ni takribani vijimyaka kadhaa sasa vimeishaenda magharibi taangia nimeanza kufuatilia kwa ukaribu mno jinsi na namna ambavyo board ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini inavyotenda kazi zake.Nilichokibaini juu ya shughuli na utendaji kazi wa HESLB ni madudu matupu tena zaidi ya yale walioyabeba wao wenyewe wanaojiita watendaji wa HESLB.

Hainiingii akilini hata kidogo nadhani hata wewe unayeisoma hii mada haikuingii akilini kuona HESLB inawapa mkopo wanafunzi ambao ni watoto wa viongozi na wengine wazazi wao ni wafanyabiashara wakubwa wanaoshirikiana na watawala wa taifa hili huku ikiwatelekeza wanafunzi ambao ni yatima na wengine ni watoto wa akina pangu pakavu tia mchuzi.

Kwa mfano asilimia kubwa ya wanafunzi waliokuwa wamesimamishwa masomoni pale UDOM mnamo mwaka wa jana ni mayatima na wengine wametokea katika familia duni,cha kushangaza,kuhuzunisha na kusikitisha HESLB bado mpaka sasa haijawapatia watoto hawa stahiki yao (fedha za kujikimu).Hii sio haki.

Nina swali moja kwa watendaji wa HESLB,JE NYIE WATENDAJI WA HESLB MMEZAA NA JE MNAUTAMBUA UCHUNGU WA MWANA?? Nasema acheni ubabaishaji na wapeni watoto pesa kwani ni haki yao ya msingi.Nasema tena acheni kufanyia miradi pesa za hawa wanafunzi.Hili ni zimwi kwakweli.Naomba kuwasilisha.
 
Nadhani board ninavyo jua ni kama miungu hapa Tanzania.Akuna haki kwa masikin,Watumishi wanajibu watu vibaya.Mungu tuongoze tupate Tanzania mpya tuitakayo.
 
Hivi tujiulize waliochukua mikopo huko nyuma,ni wangapi wamerudisha kwa hiyari au hata kwa kulazimisha?Wanafunzi wakipewa mikopo hawarudishi,hii inafanya board inakua na hali ngumu sana.Mi nadhani elimu ya Tanzania iwe bure kuanzia chini hadi vyuo vikuu vya uma.Hii itaondoa matabaka.Wale wa vyuo binafsi viwe na utaratibu wa mikopo.
 
kaka inauma ile baya tena mbaya zaidi inawapa mikopo watu ambao wamesoma shule zenye karo kubwa mfano feza na vinginezo kisa wamenasoma facult kipaumbele na wale watu waliosoma shule za kata wananyimwa mkopo kisa hawasomi facult kipaumbele..kiukweli inauma sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…