Zinadine zidane:chrismass yako iko karibu..

Zinadine zidane:chrismass yako iko karibu..

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Ni kama vile hadithi ya kufurahisha, kijana anapokuwa Chuo, yeye na wenzake wataanza kujipangia kuwa baada tu ya kumaliza chuo, basi watapata kazi na moja kwa moja atakuwa CEO!

Lakini Kumbe alikosea sana, alikosea sana kwa kuyachukulia mambo kirahisi mnoo..

Zinadine zidane ni mmoja wapo.
Alidhani mara zote mambo huwa mepesi!. lakini Kumbe alikosea!..

Alipokuja kwa Mara ya kwanza, alikabidhiwa team b..
Baada ya muda akapatiwa team ya wakubwa na tunajua mafanikio aliyoyapata .

Nafikiri zidane hakujua au alijua ila akapuuza,
Kikosi kile kilichobeba UEFA tatu mfululizo kilikuwa na mengi.

Kwanza wachezaji wake walikuwa wapo kwenye ubora wao kutokana na kuzoeana vizuri,
Pili wachezaji wale umri ulikuwa umeenda nusu ya wote..

Nafikiri ungenikurupua usingizini ningekutajia kikosi kile chote kipa mpaka mshambuliaji!

Ilikuwa kikosi kimezoeana kwa kucheza muda mrefu..kulikuwa na chemistry ndani yake, alichofanya zidane ni kuwapa confidence tuu.. na alijua wazi kikosi kile kisingeweza kukaa misimu miwili inayofuata..

Alifanya la maana Sana alipoondoka nami nilifurahi maana alikwepa matatizo,

Ndiyo,matatizo kama florentino Perez...mwanadamu anayeamini kupata tuu na sio kukosa!.

Kosa alilofanya ni kurudi tena pale kwenye viunga vya Santiago bernabeu!..
Kurudi sio kosa, kosa ni alirudi akiwa hana uhakika atajenga kikosi gani tena cha ushindani!.

Alidhani mambo ni rahisi kama zile chenga maridadi alizokuwa anapiga!..

Sahau ile aibu aliyoipata mbele ya maelfu ya mashabiki pale mbele ya watoto wale wa Diego simeone "chollo " sahau!

Mtu kama Garry nevile..
Mchezaji nguli anayeheshmika uingereza,, nae akadhani kufundisha ni sawa na kucheza!

Hakujua kufundisha ni zaidi ya soka lenyewe, ni kazi nyingine tofauti kabisa! kwa sasa hataki tena kufundisha, anajua jinsi kazi ilivyo..amekuwa mchambuzi.

Claurence sedorf
Thienry Henry wanajua jinsi ukocha ulivyo!

Achilia mbali Frank Lampard ambaye ameanza kuelewa jinsi kazi ilivyo..

Kwa sasa Perez hana lawama tena,
Yes ametoa fungu kubwa la usajili,katimiza wajibu wake
Alichobaki ni kusubiri zidane amletee makombe yakae kabatini.. Yes!

Nadhani mpaka kufika Christmas tutashuhudia mengi ikiwemo hili la zidane..

Pengine pia zidane anaweza kuwa mtu ambaye anaomba Christmas isifike maana ndio kipindi makocha wengi wanapokonywa tonge mdomoni!
Zidane Christmas ipo karibu!...

Pancho boy
 
Huyu Zidane wala hatafika mbali,mtaniambia.Labda wakifanikiwa kumnunua Neymar .
Neymar simpi nafasi hata kidogo.
kwanza Neymar soka lake amateur sanaa
na zizzou apendagi mchezaji awe amateur Sana that's why kuchukua Hazard na Luca jovic..

Neymar wa sasa anacheza mechi 10 kisha anaumia. na kukaa nje miezi miwili!.. Kama sio mmoja!
 
Zidane anakazi ngumu sana kuamsha ari ya wachezaji waliovubjika moyo nakupoteana
 
Kwangu zidane ni kocha mzuri tena wa viwango vya juu, kurudi madrid si kitu ambacho mie nakiafiki nilipenda abaki juventus, nadhani baada ya allegri kusepa angepewa timu yeye na kwa juve ile angefanya maajabu mengine.. kwa madrid hii tusubiri muda utasema..

Kwa thierry henry mie sioni kama monaco ilimshinda ni vile timu ile imeshajifia, monaco walijichimbia kaburi wenyewe takribani wachezaji watano ama saba wa kikosi cha kwanza waliuza, mendy,silva,mbappe,fabinho,bakayoko
Unategemea maajabu gani kwenye soka huyo jadim mwenyewe timu ilimshinda wakampora wakampa th14 akajitahidi kidogo kilichomponza ni kashfa na henry angewatengenezea ile timu vizuri, kuna wachezaji alikuwa anasajili kwa jina lake tu sio timu, kama cesc fabregas alienda monaco kwasababu ya Henry.
 
sawa kiongozi
 
Back
Top Bottom