Zinanishangaza ndoto hizi??

Unbounced

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
345
Reaction score
434
Wakuu mimi kuna wakati huwa napatwa na ndoto za mambo Ya kuuzunisha sana ambayo hupelekea moyo kuwa na maumivu na uchungu mkali.
Sambamba na hayo pia nakua natoa machozi hadi shuka inalowa na inadumu Kwa muda mrefu kiasi kwamba hata nikistuka toka usingizini machozi huwa yanaendelea kutoka na moyo unakuwa na uchungu wa hasira ambao kiuhalisia sijawai kuwa na hali kama hiyo katika hali Ya kawaida. Pia nakuwa natetemeka Kwa hasira na hunichukua muda sana hadi kuwa kawaida baada Ya kutoka usingizini. Kiukweli inanishangaza sana hali hii na si mara nyingi kutokea,inaweza tokea mara tatu Kwa miez sita .wataalamu wa saikolojia, imani na wataalam wa maswala ya utendaji kazi wa ubongo pamoja na wote wenye ufahamu na jambo hili naombeni mnisaidie mana nazichukia hizi ndoto hasa kunipa hasira ambayo katika hali Ya kawaida sijawai kuwa nayo
 
fafanuwa zaidi jinsi unavyo ota hizo ndoto za kuhuzunisha ni ndoto za aina gani hizo?
 
fafanuwa zaidi jinsi unavyo ota hizo ndoto za kuhuzunisha ni ndoto za aina gani hizo?
Ndugu yangu Mara kadhaa huwa nakumbuka ni ndoto za vifo vya watu muhimu sana kwangu na wakati mwingine huwa sikumbuki ni tukio gani linanifanya kuwa na huzuni ila nakumbuka huwa ni vitu vya kutisha na kuogofya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…