Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,395
- 2,391
Ni siku nyingine tena nakuja kivingine, Natumai mko powa wasomaji.
Leo nataka kuwapa mbinu za kukabiliana na matapeli sababu hawaishi na kila siku wana mbinu mpya.
Kwa sasa mawakala ndio wanaongoza kwa kutapeliwa kupitia wateja wao kivipi? Twende pamoja kwenye makala hii.
Kwanza kabisa kuna utapeli wa aina mbalimbali,wa kwanza tapeli anaweza kujua taarifa au tabia zako kiasi kupitia rafiki yako au ndugu yako na akazitumia kutumiza lengo lake.
Pili matapeli wengi kwa sasa wanajua wengi wa raia hawana pesa nyingi kwenye simu zao kwa hiyo wanawatumia kutapeli mawakala. Huu ndio utapeli 🔥 kwa sasa.
Iko hivi, anaweza kuja mteja wako,jirani yako,mpangaji mwenzako ambaye unamjua vizuri kabisa na huna shaka nae, akiongea na simu akiwa na namba na jina kwenye karatasi akitaka umtumie kiasi fulani cha pesa. Kwa haraka hutakuwa na mashaka nae sababu ni mteja wako(jirani, rafiki) kulingana record zenu za nyuma. Akiwa bado simu iko hewani tapeli akihakikisha hampi nafasi ya kushauriana na wakala kabisa ili asije akashtukiwa.
Miongozo na semina toka kwenye makampuni ya simu ni kwamba
1. Muwekee pesa mteja ambaye yuko na simu yake hapo hapo.
2. POKEA PESA HESABU PESA TUMA PESA. n.k
Sasa hapo utachukua simu na kutuma pesa kwenye namba uliyopesa na mteja wako. Baada kutuma atakwambia kuna hela imetumwa huku kwangu na hapo mtaanza kutoa kwenye simu ya mteja wako sasa. Mtatoa na pesa haitatoka sababu hakuna salio(kumbe ni meseji ya kufoward au ya kawaida) sio ya pesa.
Tapeli anazima simu anawaacha mkigombana wewe na mteja wako sababu.
WAKALA USITUME PESA KABLA HUJAPOKEA PESA(ACHANA NA MAZOEA)
Nina visa zaidi ya vinne nimeshuhudia mwenyewe wateja wawili niliwasaidia mimi na wengine mawakala wapigwa pesa ndefu sana. Nitatoa kimoja kiwe funzo na ushuhuda.
KISA CHA KWELI KWANGU
Alikuja mpangaji mwenzangu akiongea na simu,huyu namjua sana tunakaa nyumba 1 na pesa zake anatumaga kwangu na kutoa kwangu hata kama sina float atanisubiri au atatoa kisha baadae atafata pesa yake, kwa hiyo swala la kuaminiana ni 💯 mimi na yeye. Mazungumzo yalikuwa hivi:
Jirani: braza una salio kwenye voda?
Mimi: kiasi gani?
Jirani: kama 340,000.
Mimi: ndio ipo
Jirani: naomba unitumie kwenye namba hii(ananipa karatasi huku simu yake ikiwa kwenye sikio)
Mimi: naomba hela nihesabu kabisa.
Jirani: nakupa ipo kwenye simu hii naongea nayo.
Mimi: kata simu kwanza(nahitaji ufafanuzi zaidi)
Jirani: hapana huyu jamaa naongea naye kasema nisikate simu mpaka hela itumwe.
Mimi: nikashtuka kidogo!! Nikauliza ni nani?
Jirani: labda uongee nae(akanipa simu)
Mimi: mambo vip?
Simu: safi nsugu yangu,anatoa maelezo marefu ya kukosea muamala ukaja kwa jirani yangu kiasi cha 390,000 lakini akitaka kurudiahiwa 340,000 tu hiyo 50k ni ya usumbufu.
Mimi: kwanini asikurudishie kupitia simu hii hii bila kutumia wakala?
Simu: hapana kaka,ukitumiwa pesa na kurudisha kwa namba iliyotuma huwa inachelewa kufika ndio maana nataka itumwe kwa wakala moja kwa moja kisa yeye atoe hapo kwako, nisadie ndugu yangu.
Nikampa jirani simu nikamwambia kata hiyo simu. Akadai ameambiwa asikate mpaka hela itumwe (kwa kitisho cha kublokiwa namba na kutafutwa popote alipo).
Mimi: KATA SIMU HIYO. Kweli akakata simu na nikwambia huyo tapeli kama ni kweli basi tutoe hiyo hela ikitoka tumtumie. Ukweli hakua na hela ila msg ya kutimwa lakini sender ni namba ya kawaida imeseviwa M-PESA.
Jirani yangu hakuamini,kesho alikuja kunishukuru sana na kusema kama ningetuma angelipaje? Hakulala usingizi akijiuliza maswali tu.
MWISHO.
Kama ningechukulia poa kwamba "huyu namjua ngoja nitume tu" nani angepata hasara? Ni jirani yangu lakini sikutumia mazoea,nilitimia kanuni za kazi.
Ndugu wasomaji kuweni makini mnapoona fursa ya haraka isiyotumia nguvu kubwa,wala muda kuipata. Huenda ikawa wewe ndio fursa yenyewe.
ASANTENI. Kama umepata elimu kidogo kupita makala hii sio mbaya ukanipa kura yako.