Zingatia haya ili uweze kupata au kushinda Tender mbalimbali

Zingatia haya ili uweze kupata au kushinda Tender mbalimbali

DALALI MKUU

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2022
Posts
2,011
Reaction score
4,705
Nyaraka za zabuni (Tender documents) ni mkusanyiko wa nyara-ka zinazoandaliwa na taasisi nunuzi kwa lengo la kuwaalika wazabuni wenye sifa za kushiriki katika mchakato wa zabuni ambapo hatimaye mmojawao hupatikana na kupewa tuzo ya mkataba.

Sehemu kubwa ya maelezo yaliyomo kwenye nyaraka za zabuni, huzingatia matakwa ya sheria ya manunuzi ya umma na kanuni zake. Aidha, kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma, taasisi nunuzi zinatakiwa kutumia nyaraka sanifu (standard tender documents) ambazo hutolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma.

Katika kufuatilia kwangu masuala hayo nimegundua kwa kiasi kikubwa wazabuni wamekuwa hawazingatii masharti yaliyowekwa kwenye kitabu cha nyaraka za zabuni na hivyo kuchangia kwa sehemu kubwa kukosa au kushindwa katika kinyang’anyiro cha zabuni hiyo.

Vitabu vyenye nyaraka za zabuni vimewekwa katika makundi tofauti kufuatana na aina ya ununuzi unaotakiwa kufanyika. Makundi ya ununuzi Manunuzi ya umma yamegawanyika katika makundi makuu yaVifaa/bidhaa, kazi za majenzi, huduma zisizohitaji ushauri wa kitaalam na Huduma za ushauri wa kitaalam.

Vivyo hivyo, nyaraka sanifu za zabuni zitolewazo na PPRA zimeandaliwa kulingana na makundi hayo. Sehemu kuu za kitabu cha zabuni ni:

I. Mwaliko wa kushiriki zabuni(Invitation for Tenders)
II. Fomu ya zabuni (Form of ten- der)
III. Maelekezo ya jumla kwa waz- abuni (Instructions to tenderers)
IV. Maelekezo maalumu kwa wazabuni (Tender data sheet)
V. Masharti ya jumla ya mkataba (General conditions of contract)
VI. Masharti maalumu ya mkata- ba (Special conditions of contract)
VII. Fomu ya usalama (Forms of security)

Hivyo, wazabuni wanaoshiriki michakato ya zabuni za umma, wanapaswa kuhakikisha kuwa wanajaza nyaraka hizi ipasavyo na kuomba miongozo kwenye taasisi nunuzi husika au PPRA ili wasipoteze nafasi ya kupata zabuni kwa kukosea kujaza nyaraka, licha ya kuwa na sifa na vigezo vya kutekeleza zabuni husika.
 
Mkuu heri? Naomba kuuliza, ni nyaraka Gani muhimu nazihitaji kujiunga na Nest, na ni gharama Gani ya fedha inahitajika?
 
Mkuu heri? Naomba kuuliza, ni nyaraka Gani muhimu nazihitaji kujiunga na Nest, na ni gharama Gani ya fedha inahitajika?
inategemea na aina ya Biashara, n.k ila ukitaka kujiunga unaingia kwenye mfumo wakati una register inakuonyesha aina ya baishara yako ni shilling ngapi. ita Generate control number na utaona kaisi unachotakiwa kulipia ila kwa local company ni 100,000
 
Kwa ambao tumewahi kufanya kazi na waomba zabuni, rushwa imetawala sana. Wengine huanza kazi hata kabla ya kutangaza zabuni. Wanaofuata tararibu huhalalisha tu mchakato wa manunuzi, anayepata ni mwenye kuhonga na kujuana (connections), hata kama hana vigezo au vifaa vya kufanyia kazi.
 
Kwa ambao tumewahi kufanya kazi na waomba zabuni, rushwa imetawala sana. Wengine huanza kazi hata kabla ya kutangaza zabuni. Wanaofuata tararibu huhalalisha tu mchakato wa manunuzi, anayepata ni mwenye kuhonga na kujuana (connections), hata kama hana vigezo au vifaa vya kufanyia kazi.
Ulishawahi kutumia huu mfumo mpya wa nest au unazungumzia ule wa Taneps? jifunze kidogo uone mfumo wa nest ulivyo na uwazi mkuu.

Ila mbinu chafu kwenye kila eneo hazikosekani, ila sio sababu ya kuacha kufanya jitihada kwa hofu ya rushwa au kujuana.

Michezo michafu ipo kila sekta
 
Nest imepunguza muanya wa kujuana na rushwa, japo bado ipo, na ndio maana kuna kasoro kwenye tender awards na wanapelekwa public procurement appeal authority na wanatengua award.

Bado tunasafari ndefu. Nest inatakiwa kuonesha ufunguzi na nani kapewa hio tenda na kwa bei gani iwe wazi kwa watu wote sio walioshiriki tu, itaongeza transparent.
 
Kwenye NEST unapigiwa simu ""Umeomba nikuchague""
Kujuana kupo palepaleeee.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
hizi ni kauli za kuwakatisha tu tamaa wapambanaji waogope kuomba tender. Mimi najua vizuri sna hii mifumo maana ni kitu kila siku nafanya
 
Kuwa mkweli,nest hutoa taarifa ta award,na kiasi pamoja na sababu ya wewe kukosa
 
Back
Top Bottom