Zingatia haya kabla ya kuanzisha biashara mtandaoni

Zingatia haya kabla ya kuanzisha biashara mtandaoni

Joined
Mar 11, 2022
Posts
14
Reaction score
15
Watu wengi sana wana anzisha Biashara Mtandaoni, Wapo wanaofata Kanuni zake, na ndio maana wanafanikiwa na wengine Hawafati na wala hawazijui.

Kanuni Hizi ni kabla ya kuanzisha Biashara Mtandaoni, unatakiwa uzifahamu ili kufanikiwa katika Biashara yako.

1. Wazo La Biashara.

Hapa Unatakiwa Uwe makini Kuchagua wazo zuri la Biashara ambayo itakulipa.

LENGO kuu la Biashara Ni Kutatua Changamoto Furani ya Watu na wakakulipa Pesa.

Kaa Chini Fikiria , nifanye Biashara gani ?

Chukua karatasi, Andika kila wazo ulilopata, kisha Fanya Mchanganuo wa mawazo hayo.

Nb. Hakikisha Unaandika Wazo lako utakalokuwa umepata, Andika Andika Kwa Ufasaha Biashara yako Ni Ipi.

2. Jina La Brand Yako. ( username )

Kwa Kuwa Tunajadiri Biashara za Mtandaoni, Swala la jina la Brand yako ni Muhimu sana,

Wataalamu wanasema " Your Brand name Must be Simple and Unique"

Usichague jina la hovyo tu ilimradi. Chagua jina Ambalo ni Fupi na ambalo ni Rahisi mtu kukumbuka pale anapotaka kukutafuta.

Ukishapata Jina lako, Mfano, "Seifu Pamba Kali"

Hakikosha Jina hilo Moja Kwa Herufi Hizo hizo linatakiwa kutumika Mitandao yote ya kijamii.

Kama Mfano

Instagram #Seifu Pamba kali
Facebook #Seifu pamba Kali
Twitter. #Seifu Pamba Kali
You Tube #Seifu Pamba kali

Sio Mtandaoni Huu unatumia Jina lile na Mtandao huu unatumia jina Hili. Hakikisha Hadi Email yako majina yanafanana.

3. Security ( Usalama )

Hakikisha Unaweka Password imara na kufata hatua Zote za kiusalama Ambazo mtu Hawezi kukudukua ,

Siku hizi kuna wezi wa Account za Watu , hakikisha unaimarisha Usalama wa kutosha wa Password na Kuweka "Two Factors Of Authentication"

Ukimaliza Hizo Hatua 3, Sasa Anza kutengeneza Contents ( Post ) Zako na kupost kila siku bila kukata Tamaa.

Official seifu

Dar es salaam, Tanzania [emoji1241]

+255 788 100 190
Adobe_Express_20220712_1339480.25963823280047194.jpg
 
Back
Top Bottom