Zingatia haya wakati unafikiriaa kujenga, yatakusaidia

MoseeYM

Senior Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
144
Reaction score
199
Naomba kuwakumbusha wale mnaoanza au mnaotaka kujenga.

Mtambue ya kuwa katika ujenzi 60%-70% ya gharama utakayotumia kwenye ujenzi,Mara nyingi huwa ni gharama ya material. Kwa hiyo usijisumbue kutumia 'mafundi maiko' wahuni ,wakujengee kwa kisingizio cha kusave gharama za wataalamu,Hiyo 30%-40% unayoipigania inaweza kuigharimu 60%-70%.

Ukweli mchungu ni kwamba,nyumba nyingi za makazi zina changamoto ya 'ubora'.Unakuta mtu alikwepa kutumia wataalamu kukwepa 1M.Baadae 'as a consequences' kila mwaka anafanya marekebisho yenye gharama kubwa.

Kitaalamu 'life span' ya majengo tunaexpect iwe 50years or more with slightly maintenance.Lakini hizi za kwetu 10yrs nyumba unakuta imechoka tayari.Au unakuta gharama za marekebisho alizotumia mtu,angeweza kujenga hata nyumba nyingine.

NI MUHIMU KUZINGATIA ubora na ushauri wa wataalamu unapoanza ujenzi.Suala la gharama sio la kuhofia kwa sababu bado Tanzania tunao wataalamu wengi wanaoweza kukushauri namna bora ya ujenzi kulingana na kiasi Ulichonacho( Mfano kuna watu wanaitwa Quantity surveyors ,kazi yao ni kufanya ukadiriaji wa gharama za ujenzi, Wahandisi ujenzi nao wapo,ambao miongoni mwa kazi zao kubwa ni kusimamia ubora wa materials na namna ya ujenzi,Pia hufanya design.Wapo Ma -Architects kazi yao ni kufanya usanifu wa majengo.

SIJAJUA WABONGO TUNAKWAMA WAPI? Ila taratibu tutazoea.
 
Mtambue ya kuwa katika ujenzi 60%-70% ya gharama utakayotumia kwenye ujenzi,Mara nyingi huwa ni gharama ya material. Kwa hiyo usijisumbue kutumia 'mafundi maiko' wahuni ,wakujengee kwa kisingizio cha kusave gharama za wataalamu,Hiyo 30%-40% unayoipigania inaweza kuigharimu 60%-70%...

Ulisema kweli. Umetumia wewe wataalamu kwenye ujenzi wako ?
 
Naomba kuwakumbusha wale mnaoanza au mnaotaka kujenga.

Mtambue ya kuwa katika ujenzi 60%-70% ya gharama utakayotumia kwenye ujenzi,Mara nyingi huwa ni gharama ya material. Kwa hiyo usijisumbue kutumia 'mafundi maiko' wahuni ,wakujengee kwa kisingizio cha kusave gharama za wataalamu,Hiyo 30%-40% unayoipigania inaweza kuigharimu 60%-70%...
Nzuri asante mkuu
 
Kaka Tanzania zaidi ya 70% wanaishi kwenye poverty line,na bado hao 30% wanao baki ndio hao wafanyabiashara+Wafanyakazi ambapo vipato vyao ni vya kubangaiza kwa ajili ya kula.Hivyo wengi wanajenga kuondoa aibu katika Jamii kwa kuwatumia funding Maiko.
 
Kama ulinielewa vizuri.

Kuna sehemu nimezungumza kwamba,tunao wataalamu wwngi wanaoweza kukushauri kujenga nyumba nzuri na kwa ubora kulingana na kiwango chako.

Nadhani humu kuna wataalamu wa masuala ya ujenzi.
Miongoni mwa vitu tunavyofundishwa vyuoni ni :kuwa 'economical' kwa maana ya kwamba usilete gharama ambazo ni unnecessary.Lakini pia msisitizo wa vyuo vingi hapa kwetu vinavyofundisha haya masuala ni kuwa 'economical' ili kuendana na hali ya kiuchumi ya watu
 
Yes,
Mimi pia ni mtaalamu wa masuala ya ujenzi (Mhandisi ujenzi).
OK, niambie, unafikiri kuhusu post hizi zangu Ningetaka kujua maoni yako. Unafikiri kama nchini tunaweza kufanya hyvio na bei bora ?

Yes,
Mimi pia ni mtaalamu wa masuala ya ujenzi (Mhandisi ujenzi).

Ok ndg mhandisi sorry ninaomba nikuulize swali la ufahamu. Ninahitaji kufahamu kazi ya Architect inaishia wapi na nyie wahandisi kazi yenu inaanzia wapi kwenye usanifu wa jengo mpk ujenzi na kukamilika kbs?
 
Kazi ya architect kiufupi huishia kwenye mpangilio na muonekano "Architectural drawings'. Lkn kwa mhandisi ujenzi (Structural Engineer) kazi yake ni kuandaa design ya ndani au skeleton (Structural drawings) ambayo hii hujumuisha mpangilio wa nondo na vinginevyo.Lakini hawa wote hufanya kazi bega kwa bega mpk kazi inakamilika.

Mfano: Architect akishaandaa michoro yäke,anaipeleka kwa Engineer ili naye aandae michoro yake kulingana na kile architect alichokisanifu.Endapo kutakuwa na mabadiliko hawa watu hushauriana
 
Kiufupi Tasnia ya Uhandisi ujenzi nayo imegawanyika.

Kuna "Structural Engineers' wao wanahusika na ujenzi na design ya vitu kama vile Majengo na madaraja.

Kuna " Highway Engineers " na "Transportation Engineers" hawa wanahusika na mambo ya barabara.

Kuna "Material Engineers" or "Geotechnical Engineers" wao huhusika na mambo ya materials ya ujenzi.

Pia kuna "Water resources Engineers" or 'irrigation Engineers" wao huhusika na mambo ya maji na miundombinu yake
 
Geotechnical ni mtu ana deal na miundo mbinu iliyopo ardhini mfano misingi, tunnels etc etc! Hawa wanajua kiundani zaidi jinsi jengo au structure inavyo interact na ardhi.

Nadhan utofautishe geotech eng na highway eng...
 
Uko sahihi.

Hapo niligeneralize tu.
 
Naomba kuwakumbusha wale mnaoanza au mnaotaka kujenga.

Mtambue ya kuwa katika ujenzi 60%-70% ya gharama utakayotumia kwenye ujenzi,Mara nyingi huwa ni gharama ya material. Kwa hiyo usijisumbue kutumia 'mafundi maiko' wahuni ,wakujengee kwa kisingizio cha kusave gharama za wataalamu,Hiyo 30%-40% unayoipigania inaweza kuigharimu 60%-70%.

Ukweli mchungu ni kwamba,nyumba nyingi za makazi zina changamoto ya 'ubora'.Unakuta mtu alikwepa kutumia wataalamu kukwepa 1M.Baadae 'as a consequences' kila mwaka anafanya marekebisho yenye gharama kubwa.

Kitaalamu 'life span' ya majengo tunaexpect iwe 50years or more with slightly maintenance.Lakini hizi za kwetu 10yrs nyumba unakuta imechoka tayari.Au unakuta gharama za marekebisho alizotumia mtu,angeweza kujenga hata nyumba nyingine.

NI MUHIMU KUZINGATIA ubora na ushauri wa wataalamu unapoanza ujenzi.Suala la gharama sio la kuhofia kwa sababu bado Tanzania tunao wataalamu wengi wanaoweza kukushauri namna bora ya ujenzi kulingana na kiasi Ulichonacho( Mfano kuna watu wanaitwa Quantity surveyors ,kazi yao ni kufanya ukadiriaji wa gharama za ujenzi, Wahandisi ujenzi nao wapo,ambao miongoni mwa kazi zao kubwa ni kusimamia ubora wa materials na namna ya ujenzi,Pia hufanya design.Wapo Ma -Architects kazi yao ni kufanya usanifu wa majengo.

SIJAJUA WABONGO TUNAKWAMA WAPI? Ila taratibu tutazoea.
Na kudownload ramani kwenye mtandao afu anampa fundi Michael anaifanyia maboresho ya kihuni kihuni.

Ila wengi hata hawanunui ramani hajui nyumba hadi inaisha itaezekwaje anaishia kumuachia fundi abuni paa matokeo yake unakuta nyumba zote zinafanana hakuna hata uniqueness.
 
Kuna kiwanja nilipata kiko kwenye udongo wa mfinyanzi. Fundi ameniambia bila msingi wa nondo na zege nitegemee ufa muda mfupi ujao.
 
Hiyo ni Kwa sababu udongo mfinyanzi unaasili ya kusinyaa na kutanuka ukipigwa na jua.hiyo hupelekea mipasuko inayoathiri mpk nyumba. Ingawaje zipo namnanyingi za kupambana na mfinyanz.
Mfano kuna wengine udongo WA kurudishia huchanganya na chokaa, cement aumchanga kureduce shrinkage ya udongo inayoweza athiri msingi.

Thus why hata ujenzi WA barabara chokaa au cement huchanganywa na udongo
 
Na kudownload ramani kwenye mtandao afu anampa fundi Michael anaifanyia maboresho ya kihuni kihuni.

Ila wengi hata hawanunui ramani hajui nyumba hadi inaisha itaezekwaje anaishia kumuachia fundi abuni paa matokeo yake unakuta nyumba zote zinafanana hakuna hata uniqueness.
Hilo nalo ni tatizo
 
haya mambo ya PDF, hao unaowaita wataalam utawapa kazi nao pia watawapa kaz mafund wengine..na mataalam wako akijisahau tu wataharibu nyumba vilevile,mafundi wazuri wapo wengi kikubwa usimamizi tu.
 
Back
Top Bottom