Zipi hatua za kisheria za kuchukua juu ya hospitali kwa uzembe kwa mgonjwa

Shoo Gap

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
261
Reaction score
97
Kwanza, niwapongeze Wahudumu wa afya wenye moyo wa dhati na wanaozingatia taaluma na uadilifu kuhudumia wateja wao. Nakiri maisha ya wengi ikiwemo mimi binafsi yana mchango wa wahudumu wa afya.

Hata hivyo, nimekutana na matukio kadhaa ya makosa ya uzembe wa wazi wa baadhi ya wahudumu wa afya.
MIFANO MIWILI
1. Ndugu yangu alilazwa Hospitali Maarufu ya Rufaa nchini akiwa na complication ya ujamzito ikiwemo BP kuwa juu. Ilitokea tukio moja ambapo aliandikiwa dawa na kushusha BP lakini dawa aliyopewa ni ya kupandisha BP. Ashukuriwe Mungu yeye binafsi ana ujuzi wa hizo dawa kwa hiyo baada ya Nesi kumpa ili ameze alishtuka na kubaki amezishika akiwa amepigwa na butwaa kwa dakika chache. Ghafla akatokea Nesi mwingine akamfuata na kumuuliza mbona humezi dawa. Akamwangalia na kumkabidhi zile dawa na daftari la taarifa zake. Yule Nesi alishtuka sana na kuwafuata wenzake kwa kasi kisha wakaja kwa pamoja kama watano hivi na kumzunguka. Baada ya kumwuliza maswali kadhaa walienda kubadilisha zile dawa na kumletea dawa anayostahili. Ebu fikiria asingekuwa na uelewa wa hiyo dawa au angekuwa hajitambui.

2. Wiki iliyopita kuna rafiki amefariki baada ya kufanyiwa operesheni 4 za tumbo kwenye Hospitali ya rufaa. Tangu awali tulishaona kuwa wanachofanya ni kana kwamba wanabatisha na tuakawaomba watoe rufaa kwenda Hospitali nyingine LAKINI KILA MARA WAKAWA WANAKATAA. Pamoja na kwamba kifo kina mpango wa Mungu lakini unaona dalili zote za kutowajibika ipasavyo.

SWALI: NI TARATIBU GANI ZA KISHERIA ZA KUCHUKUA KUIWAJIBISHA HOSPITALIA AU MHUDUMU WA AFYA KWA UZEMBE WA WAZI JUU YA MGONJWA? AIDHA, NI HATUA GANI ZA AWALI MGONJWA ANAZOPASWA KUCHUKUA KUMWEZESHA KUKUSANYA USHAHIDI UTAKAOWEZA KUMLINDA KISHERIA?
 
Nadhani kila hosiptali (kubwa) inapaswa iwe na bodi ya kuchunguza uadilifu na utendaji kazi wa wauguzi na madaktari..
 
katoe lalamiko kwenye Medical Council of Tanganyika, huwa wanawafanyia mashtaka kama sikosei. hilo ni balaza la madaktari Tanganyika.
 
Back
Top Bottom