Sina group lolote la whatsapp kwenye simu yangu mbali ya yale ya ofisini ambayo yapo sababu ya uendashaji wa kazi wa kila siku.
Naamini siku zote kila hatua ya maisha unayovuka unapaswa kuiacha huko huko ulipotokea. Sio usahau uliokuwa nao, hapana, achana nao kimazoea unless kuna uhitaji.
Naamini magroup yote ya shule na vyuo ulivyopitia huwa hayana dhamira ya kutaka kusalimiana na kujuliana hali. Yapo pale maalum kupima mafanikio ya walio kwenye group.
Binadamu tuna kawaida ya kukadiria heshima tunayompa mtu kulingana na aidha uwezo wake kiuchuni, madaraka yake ama uhitaji wako kwake.
Ukija kwenye magroup ya ukoo, hayo ndio ya kuepuka kabisa. Daima hakuna adui mbaya kama yule mwenye nasaba na wewe. Katika hayo magroup kuna wajomba, mashangazi, binamu nk. Sio kila ndugu atafurahia maendeleo yako ikiwa yeye ama mtoto wake hana mafanikio. Na si kila ndugu atakuwa na huruma na dhiki zako.
Kupitia hayo magroup, kwanza kuna wale wa kukadiria uwezo wako wa pesa kutokana na shughuli zako, watakuomba msaada, ukisema huna utaambiwa una roho mbaya. Mwanzo wa husda ndio huo sasa.
Daima naamini, mwenye uhitaji na mimi iwe ndugu ama rafiki lazima atakuwa na njia ya kunipata lakini njia hiyo isiwe magroup ya halaiki. Na kama kuna taarifa inapaswa niipate, nitaipata tu.