nunua kiwanja kwa mwenyeji kabla hujalipia ita majiran zako wote mnaopaka nao muhakiki mipaka ni sawa? na wasaini hati ya mikaka. ishu kumbwa ni hapo kwa mipaka mimi ndo nilikumbana nayo
Hakikisha muuzaji ndiye mmiliki halali
Omba hati halisi ya umiliki/Certificate of Title au nyaraka za umiliki, kisha zihakiki Ofisi ya Ardhi. Usikubali nakala pekee. Ofisi ya Usajili wa Hati husajili hati, uhamisho wa milki na rehani.
Fanya upekuzi wa ardhi (search) Ofisi ya Ardhi
Thibitisha kama kiwanja kina rehani, zuio, kesi, wadai, au kimeuzwa kwa mtu mwingine , mfano wakati mwingine unaweza Kuta kiwanja kimewekewa mkopo benki.