Zipi ni taratibu na gharama za kurenew leseni ya udereva iliyopotea

airwing

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2017
Posts
382
Reaction score
536
Habari wanajamvi.

Nilikuwa nauliza utaratibu ukoje pamoja na gharama za Kulipia, Viambatana vya kuambatanisha, Ikiwa Una leseni ya udereva ambayo ukomo wake ni 2027 na imepotea.
 
chukua loss report na 70000 nenda TRA iliyokaribu nawe
Kwenye hio 70,000 akitaka mambo chapu chapu afunikie na 30,000 kwa juu halafu amwambie naitaka leseni leo leo, chapu kwa haraka anaipata leseni yake -corrupt Country lazima uishi hivyo bila hivyo lazima apigwe nenda rudi km anafuatilia namba Nida
 
haina haja ya rushwa ma TRA wanampa control number anaenda kulipa bank au kwa simu
 
Bàada ya hapo anasubiri muda gani?
Habari wanajamvi.

Nilikuwa nauliza utaratibu ukoje pamoja na gharama za Kulipia, Viambatana vya kuambatanisha, Ikiwa Una leseni ya udereva ambayo ukomo wake ni 2027 na imepotea.
Asante kwa swali. Unachotakiwa ni kuwa na ripoti ( loss report) na utapewa control number ukalipie kiasi cha shilingi za kitanzania 70,000/= . Baada ya malipo kufanyika haizidi siku 3 za kazi kupatata. Mwisho tunawaomba sana wadau wetu na walipakodi kutokubali kutoa pesa ili upate huduma kwani huduma zetu ni bure,
 
Na ikitokea siku 3 hizo zikapita akaenda hakupata leseni achukue hatua gani nyingine?
 
Kama imepotea na muda wake
wa kuisha ni bado, hii hatuiti ku-renew, tunaita ku-dupricate. Na gharama ni ile ile.
 
Asante kwa swali. Unachotakiwa ni kuwa na ripoti ( loss report) na utapewa control number ukalipie kiasi cha shilingi za kitanzania 70,000/= . Baada ya malipo kufanyika haizidi siku 3 za kazi kupatata. Mwisho tunawaomba sana wadau wetu na walipakodi kutokubali kutoa pesa ili upate huduma kwani huduma zetu ni bure,
TRA New Vision inawezekana Lakini Maana ya Mungu mengi Na mi Nauliza Leseni yangu ya udereva imeisha toka 2016 naendesha kiujanja ujanja kwa sasa je utaratibu gani napaswa kuufuata na kuna wakati TIN Number zilibadilishwa mi sikwenda kubadili je nafanyaje?
 
Unachoandika ni kweli lakini jamii kubwà inàjua ninyi ni wala rushwa wote na hamfanyi kazi bila rushwa.
Anzeni mkakati wa kusafisha jina la TRA isiwe ina maanisha wala rushwa.
Wale wanaokuja na rushwa msipokee muwaelimishe kwamba hampokei rushwa kwa vitendo, siyo mnaandika maneno halafu zilongwa mbali zitendwa mbali!
 
TRA New Vision inawezekana Lakini Maana ya Mungu mengi Na mi Nauliza Leseni yangu ya udereva imeisha toka 2016 naendesha kiujanja ujanja kwa sasa je utaratibu gani napaswa kuufuata na kuna wakati TIN Number zilibadilishwa mi sikwenda kubadili je nafanyaje?
NASUBIRI JIBU LA SWALI HILI PIA.
TRA KUJENI HAPA WAKUU
 
Habari wanajamvi.

Nilikuwa nauliza utaratibu ukoje pamoja na gharama za Kulipia, Viambatana vya kuambatanisha, Ikiwa Una leseni ya udereva ambayo ukomo wake ni 2027 na imepotea.
70,000 tu unapata duplicate yake
 
Back
Top Bottom