Artifact Collector
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 6,617
- 10,205
Zifuatazo ni aina za akili ambazo binadamu wamekirimiwa
- Akili ya darasani, mara nyingi watu wenye akili ya darasani huwaga wanafaulu sana masomo yao na hii inatokana na uwezo wao mkubwa wa kukariri na kukumbuka na kutokusahau kile walichofundishwa
- Akili ya ubunifu, unaweza ukawa na akili ya darasan ila ukanyimwa ya ubunifu, asikuambie mtu ubunifu ni aina ya akili ambayo watu wengi sana wanataman kuwa nayo na hii ndo husababisha wengine wawe matajiri na wengine wawe watu wakawaida, na pia husababisha wengine wawe wavumbuzi na wengine wawe watu wa kawaida
- Akili ya utawala au uongozi, sio kila mtu ana akili ya uongozi mfano kuna watu wana elimu ndogo sana ila wanaakili ya uongozi, mtu kama huyu pamoja na kuwa na elimu ndogo ya darasani ni rahisi sana kufanya makubwa sana akiwa kiongozi. Na kuna watu wana akili kubwa sana ya darasani ila akili ya uongozi hawana
- Akili ya kutafuta fedha, matajiri wengi wana hii akili ya kutafuta fedha ambayo watu wengine wakawaida wanakosa na maskini wengi sana wamekosa hii akili ya kutafuta fedha
- Akili ya kumpata mwanamke, asikuambie mtu kumpata mwanamke kuna akili yake kama huna akili ya kumpata mwanamke utachezea vibuti sana, kuna watu wanakipato kidogo ila kwa sababu wana akili ya kumpata mwanamke wamejikuta wametembea na wanawake wengi sana,
- Akili ya kuishi na mwanamke, mwanaume akishampata mwanamke baada ya kumtongoza inabidi ufahamu kuna akili nyingine kabisa ya kuishi nae, tatizo kubwa sana la vijana wa leo kushindwa ndoa ni kukosa akili ya kuishi na mwanamke, na unaweza ukawa na fedha nyingi na ndoa ikakushinda sababu huna akili ya kuishi na mwanamke
- Akili ya kuishi na mwanaume, mwanamke ambaye hana akili ya kuishi na mwanaume kuwa na uhakika mahusiano au ndoa itamtesa sana, na mwanamke mwenye akili ya kuishi na mwanaume atadumu kwenye mahusiano au ndoa yake
- Akili ya kuishi na familia, ukikosa akili ya kuishi na familia nikimaanisha mke watoto na ndugu sababu familia zetu za kiafrika zinajumuisha watu wengi, sababu inayofanya mmomonyoko wa maadili ni kwa sababu wanaume na wanawake wengi hawana akili ya kuishi na familia
- Akili ya kuishi na watu, kama huna akili ya kuishi na watu utajikuta kila siku unagombana na watu