SI KWELI Zito kabwe amwambia Lissu, Kama huna hatia unagoma nini kula?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2

​
 
Tunachokijua
Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe ni mwanasiasa mahiri na mchumi nchini Tanzania, anayefahamika kwa kuwa mmoja wa waasisi na viongozi wakuu wa zamani wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo. Amewahi kuwa mmoja wa wabunge wenye ushawishi mkubwa bungeni, akitokea mkoani Kigoma.

Madai

Kumekuwa na taarifa inayosambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, inayodaiwa kutoka kwa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe, kuhusu hatua ya Tundu Lissu kugoma kula akiwa kizuizini.

Taarifa hiyo inamnukuu Zitto akisema kuwa, ikiwa Lissu anaamini hana kosa, anapaswa kusubiri uamuzi wa mahakama badala ya kugoma kula. Pia, taarifa hiyo inadai kuwa Lissu anapaswa kusubiri ahukumiwe ili hatua hiyo iwe fundisho kwa wanasiasa wengine.

Uhalisia

Hata hivyo, ufuatiliaji wa taarifa kwa njia ya utafutaji wa maenneo mhimu haujabaini chanzo rasmi kinachothibitisha kuwa Zitto Kabwe alitoa kauli hiyo.

Aidha,kupitia ufuatiliaji wa taarifa kwenye ukurasa wake wa x zamani twitter hakuna sehemo yoyote zito ametoa nukuu hiyo ambayo inasambaa kwenye mitandao

Kwa msingi huo, hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa kauli inayosambazwa ni ya Zitto Kabwe.

Sambamba na hivyo ufuatiliji bia umeanisha kuwa chombo cha habari cha Jambo tv hakikuchapisha taarifa hiyo na graphic ambayo imetumika sio halisia kama inavyopatikana hapa.

Hata hivyo JamiiCheck imewasilina na ACT - Wazalendo ambao wamekanusha pia kuhusu taaarifa hiyo na kueleza kuwa haijatolewa na kiongozi huyo.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…