Kuna katabia ka baadhi ya wanajamii humu ndani ka kutotaka kusikia wala kuona mijadala yeyote inayomuhusu mpendwa wao zitto ikiendelea,yani mnataka kumfanya zitto awe the special one humu ndani?acheni hizo!unachoshwa vipi na mijadala ya zitto ilhali bado anaishi na kuendelea kutoa kauli ambazo ndio huwa chanzo cha mijadala?acheni kumpenda zitto kupita kiasi.Duh!! Binafsi, nimechoshwa na mijadala inayomhusu zitto humu jamvini
Mbona title, body na conclusion haviendani? sema unataka kumsifia Slaa na Tindu Lisu!
Hata mimi hawa wawili nawaona safi kabisa, personally I do admire them! ila timu wanayochezea ndio ambayo haswa ina mashaka mengi sana.
Halafu sio kuwa kwa sababu unawapenda hivyo basi Lisu alipomshauri Zito basi ionekane yuko sahihi!, hakuna hiyo link! wala Kibanda hakusema lile swala kama ana lengo zuri, hapana, wao waliingilia uchaguzi wa vyama wakati ni waandishi wa habari, kw hiyo kuchukua sentensi ya Kibanda ni kumtukana Kibanda kuwa msukumo wake wa kuandika vile ulikuwa ni nini? na wewe uliomeza ile sumu, bado inakusumbua!
Slaa na Tindu Lisu! they are good ila Ni sawa na kumleta Ronadilnho au Eto achezee Yanga au Simba, next day mnamkuta Eto bagamoyo! hafanyi mazoezi wala nini anategemea bahati!
sifurahii anguko la zitto lililotabiriwa na kibanda hata kidogo. Lakini kama mtanzania ninawajibu wa kutafakari hali ya kupungua kwa mpambanaji. Hivi karibuni zitto alisema mwenyewe kuwa siasa siyo changuo lake, je hii ndiyo kuthibitisha anguko lake la kisiasa lililotabiriwa?
Kimsingi mpambanaji huyu alitakiwa kuenzi nguvu tuliyompa watanzania aliposimamishwa bungeni kwa kuonewa. Lakini polepole alianza kubadilika na alianza kwa kumpinga tindu lisu pale alipomshauri asiingie kamati ya rais ya madini. Wengi wakamwita mwanasheria huyu wa pekee kuwa ni mbinafsi kwa kumpa zitto ushauri wa kisiasa. Baadaye mbunge wetu huyu ndiyo akakoroga kabisa hadi kulumbana na katibu wake mkuu. Na kwa maoni yangu kwa sasa tindu lisu na dr. Slaa ni kati ya watanzania wa pekee waliojitoa kutetea nchi yetu, na kwa kweli wanastahili tuzo, na itakuja tu, muda utasema. Kwa mwanasiasa wa upinzani kudiriki kutofautiana na watu hao wawili, ni wazi hatutendei haki watanzania. Wamefanya mengi makubwa. Jana tumeona slaa alivyojitoa kujibu maswali hapa jf. Huyu ndiyo aina ya mtanzania kuwa rais wa nchi yetu.
Je kwa zitto kutoeleweka vizuri kisiasa kwa sasa ndiyo anguko limeshafika au amejikwaa na atasimama na kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi mkubwa katika nchi yetu unaoatamiwa na ccm?
..nadhani MMECHANGANYANA!😀either umenichanganya au umejichanganya!!
either umenichanganya au umejichanganya!!