Zitto akerwa na kauli ya Pinda

Sawa kabisa mzee maana PM wako siku hizi kauli zake zina utata mkubwa sana, tunashindwa kumuelewa hata kidogo, maana hata aseme vipi bado tunaendelea kuona kuwa CCM wanabaka demokrasia Tanzania
 

Mtoto wa mkulima hakumegewa milioni 5 za EPA wakati wa uchaguzi 2005 zilizokuwa zikitolewa kwa kila mbunge?😱
 
Hujanielewa ambaye hashauriki ni Zito siyo waziri mkuu huyo Zito wenu ameisha sema kuwa anamheshimu Pinda kifaa bwana acha majungu

Kama pinda kifaa naona kinakufaa wewe.......nyambafu!!
 

Kati yao wote wawili ni nani amesomea demokrasia? Jibu ni hakuna. Si PM wala Zitto aliye hitimu shahada ya demokrasia kwa hiyo akili ya mtu binafsi kutafsiri demokrasia ni nini ina play role kubwa hapa.

CCM haijui kitu kinaitwa demokrasia, wao wanajua serikali ni ya CCM, basi.
 
Hilo lekundu sio kweli. Hayo mengine ni mawazo yako na ninayaheshimu.

hahahaha duh haya sasa BoraMaisha umeona jibu hilo?
Unajua watu iwa hawajui mtu anaposisitiza kitu unatakiwa uongeeaje.
 
WanaJF,
Bwana Pinda amekuwa na kauli nyingi zenye utata, lakini hiyo tu inaonyesha jinsi nchi ilivyo na umasikini wa uongozi. Kwani hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa kuongea irresponsibly, mmewasahau kina Mramba(watanzania watakula majani), Msuya( kila mtu ataubeba mzigo wake), Chenge (vijisenti), Ngasongwa (mikataba kuwa siri ni best practice), hata President (ukitaka kula sharti uliwe) .Mawaziri wanawadharau wabunge hasa wa upinzani- juzi Sumari badala ya kujibu hoja za Slaa anatoa kauli za kuattack.... ''halafu na wewe tafuta hoja nyingine''. Hivi Sumari anasahau Slaa anawakilisha wananchi? Kwa tafsiri nyingine alikuwa anawakaribia wananchi wanotaka haki itendeke- to bring culprits to justice.


Anyway- to summarize, democracy is still under infancy stage (if this is not an exagerration) in Tanzania- ukitaka kujua angalia nchi za Ulaya (good example UK, people are resigning just for failing to account 5GBP!) Hapa mtu anaiibia nchi, anatukana wanachi, prime minister anasimama kumtetea tena katika bunge, na wabunge wa CCM wanashangilia!.

Hata hivyo, Zitto deserves an applause- nafurahi na kupata matumaini kwa kazi yake bungeni- tuzidi kuwahamasishana vijana tugombee nafasi- If you know kijana mwenye uwezo wa kuongoza encorage them to kugombea- tujipenyeze u taratibu one day nchi yetu itaongozwa na wazalendo!
Zitto- big up
- i like the statement aliyompa PM'.....''namshauri atazame kauli zake maana zinapelekea watu makini waanze kuhoji uelewa wake wa demokrasia,”

jioni njema wana JF- God bless us, God Bless Tanzania and Africa!
Laibon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…