Zitto amtungia Linex wimbo

Joined
Aug 6, 2014
Posts
7
Reaction score
3


Katika kuonesha ukaribu na vijana na utayari wa kutoa msaada wa hali na mali, Mbunge wa Kigoma Kasikazini Mh Zitto Zuber Kabwe amemtungia mashairi msanii wa muziki wa Bongo fleva hapa Tzee Linex Sunday Mjeda, ambaye kwa sasa kitaa anahit na single ya ‘Honga honga’.

Ngoma aliyotungiwa na Mh Zitto inategemea kutoka hivi karibuni pamoja na video yake inayo kwenda kwa jina la ‘Wema kwa Ubaya’ ngoma ambayo imetengenezwa na Maproducer 3 Mo fire Monagangstar &Tuddy Thomas. Video imetayarishwa na Adam Juma. linex amedhibitisha hilo leo wakati mwandishi wa BK alipo mcheki hewani “Nikweli wimbo wa ‘Wema Na Ubaya’ kuna mashairi kanitungia Mh Zitto Kabwe na itatoka na video yake hivi karibuni”
 
Mleta uzi acha ubo*ya@ basi!
Kwani zzito ni nani hadi umuweke jf:? Wakati kuna wengi tu huwa tunawatungia na hatujiandiki humu jukwaani!
-halafu inawezekanaje jukwaa la siasa ligeuzwe kuwa jukwaa la kupongezana kwa wachumia tumbo wachache?
Mod's fanyeni kazi na huyu kanjanja mleta uzi huu.
 
Msaliti, msaliti hafai kwenye siasa huko kwenye rusha roho anafit.
 
Aaaaaaaah!Kumbe kutunga mashairi tu...Kwanini Usiwahamasishe Kuiga Undumila Kuwili Wake..!Maana haeleweki rangi yake harisi!Sijui ACT au ccm...!kama ni Mpambe wake mwambie ajipange Upyaaaa maana amefulia..!
 
Nataka hiyo song DJ mbowe awe wa kwanza kuichea kwenye santuri(yah akumbuke enzi za bills)
 
rais wa bongo flavor...perfect,politics is not for him anymore!
 
Naam mpanda ngazi hushuka......

Na hii ni dalili moja wapo kutoka mwanasiasa nguli wa upinzani mpaka kuwatungia wimbo wasanii loh kweli usilitusi ziwa lililokunyonyesha laiti angelisikia ya wakuu......

Kesho tutasikia ooooh kaanzisha kampunii ya kuuza vitumbua kesho kitwa...ooooh sasa karudi darasani kufundisha mwisho hakutakuwa na mtu wa kumsema iwe kwa wema au ubaya...mweee usiombe mbongo akakuchukia

Mpanda ngaziiiiiiiii...............??????????

BACK TANGANYIKA
 
wamuunge kutungia nyimbo wasaniii
 
Mimi nilidhani ni uzi wa maana kumbe upumbavu...
Mods tafadhali ondoeni huu upuuzi
 
Sasa waige nn apo??? Unadhan nchi ii wote ni wasanii wa bongo flevaaa
 
Wimbo alioutunga wa majungu dhidi ya CHADEMA katika indirect way ndio cha kuiga??!!

Huyo Linex katangaza juzi atagombea ubunge kupitia ACT ya Zitto jimbo la Kasulu kwa Machali ndio Jambo la kuiga kutoka kwa msaliti??!!
 
wamuunge kutungia nyimbo wasaniii

Barray husein Obama hakuwahi kutunga mashairi ya hipo pu zitto anatungaa!!, vijana hawawezi kumwiga kwa kuwa ni mtu aliyeonyesha kuwauza,kuwasaliti na kuwafundisha kuwa kijana mwenzao hakwenda bungeni na dhamira kubwa ya kuwakomboa kutoka makucha ya chama chenye kulenga siasa za realpolitik ambazo zimelenga:
1. Kuwafanya maskini na tegemezi
2. Daima kuwa kundi la kupiga kura na si kupigiwa kura( kuchaguliwa na kuchagua)
3. Kuishi kwa kutegemea hongo la uchaguzi
4. Kunyimwa uhuru wa kutoa maoni na kukiukwa kwa haki zao za msingi kv uhuru wakujieleza,kutoa maoni,kulindwa na kupatiwa hski za msimgi kama elimu bora,mazingira bora ya kujiajiri.
Inasikitisha zitto aifwe na nani,kijana asue na msimamo,kigeugeu asiyejisimamia mwenyewe, anayeweza kujiona yeye bira kuliko wengine?
1. Kwanza hajengi teamwork ambayo katika utawala na uongozi ni nguzo muhimu katika uongozi
2. Anaweza kuwa mzuri katika ubunifu lakini si mshirikishaji
3. Hana charisma,ushahidi huu ni pale, chama chake kimeshindwa kujijenga maeneo ya kigoma na kuzalisha uasi
nitamuiga kwa lipi?
 

Asante; kwa hiyo 2015 Zitto ataibukia kwenye bongo fleva? Mhutu kwa kuiga iga mambo!... Sasa ameona Diamond katoka; Ali kiba Katoka sasa na yeye anafikiri ataweza?

Jina la kisanii ataitwaje?
Prezzo au Dogo au MM?
 
Nia yenu mnataka zzk arudi kuwalamba miguu hao wahafidhina wenu(Mbowe&Slaa)ndomana povu haliwaishi.Jueni kuwa Zzk ni Chuma cha Reli kamwe hawezi kukubali kuwa msukule kwa watu kama mbowe na slaa coz anawazidi IQ kwa kiasi kikubwa mno.
 
Nia yenu mnataka zzk arudi kuwalamba miguu hao wahafidhina wenu(Mbowe&Slaa)ndomana povu haliwaishi.Jueni kuwa Zzk ni Chuma cha Reli kamwe hawezi kukubali kuwa msukule kwa watu kama mbowe na slaa coz anawazidi IQ kwa kiasi kikubwa mno.

Ni kweli anawazidi sana kwani yeye ni msanii pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…