naamini kuwa Zito atafanikiwa ku-prove hivyo si wka maana ya kuwa hajihusishi na watu wa jimbo lake, la hasha. Zitto yu karibu sana na wapiga kura wake kuliko watu wanavyodhani. Wapo wanaoamini kuwa Mbunge kushinda jimboni ndio kuwa karibu na wananchi wakati kuwa karibu na wananchi ni kuwasaidia kutatua matatizo yanayowakabili, hata kama watakaa muda mrefu wasikuone kimwili... Zito is doing just that..binafsi ningependa Zitto awe kati wa wanasiasa ambao wata-prove kwamba dhana hizo mbili nilizozitaja hazina ukweli wowote.
naamini kuwa Zito atafanikiwa ku-prove hivyo si wka maana ya kuwa hajihusishi na watu wa jimbo lake, la hasha. Zitto yu karibu sana na wapiga kura wake kuliko watu wanavyodhani. Wapo wanaoamini kuwa Mbunge kushinda jimboni ndio kuwa karibu na wananchi wakati kuwa karibu na wananchi ni kuwasaidia kutatua matatizo yanayowakabili, hata kama watakaa muda mrefu wasikuone kimwili... Zito is doing just that
maybe Zitto (my great man) is doing but Shelukindo is not, if you want to prove waulize huko Tanga.
Mpita njia swala hili nilimuuliza mimi na naona anakujibu wewe. Nilijua huyu au anazungumza asichokijua kwa ushabiki wa Yanga na Simba au katumwa aseme PR hapa.Mpita Njia,
..mimi siyo mwananchi wa Kigoma Kaskazini. pia hakuna aliyenituma niwasemee.
..ninachojaribu kusema ni kwamba Zitto can and should juggle btn kutetea masuala ya kitaifa na vilevile awe karibu na wananchi wake.
..Kigoma Kaskazini siyo sawa na jimbo la Ubungo au Temeke. Kigoma in general iko nyuma sana kimaendeleo wanahitaji wabunge waliokaribu nao na wakereketwa wa kweli wa maendeleo yao.
NB:
..habari kwamba Zitto amelitekeza jimbo lake zilianza kutolewa na waziri mkuu Pinda bungeni.
..vilevile kuna mchangiaji wa jamii forums namheshimu sana naye alidai mambo jimboni kwa Zitto siyo mazuri.
Kwa kawaida si hulka yangu kushiriki kwenye mijadala ya kashfa kama washika dau wengine walivyofanya kwenye post inayohusu mdau Mwakalinga,lkn huwa nafanya uhakiki kabla sijaleta kitu hapa na nilichosema kuhusu harakati za mwenzetu na kugombea ubunge Kyela ni kweli tupu!
Labda ambacho sikueleweka ni kutumia tamathali za semi niliposema "Mwakalinga aingia Kyela" ukweli ilikuwa hajafika Kyela phyisical lkn "kiroho" tayari huyu jamaa alikuwa Kyela muda mrefu!
Jasusi,kuanzia tarehe 1 hadi 5 mwezi August mwaka 2009,uwepo hapa ambako nitakuletea habari moja kwa moja toka ama kiwanja cha Mwakangale-Kyela mjini,au kutoka kule kijijini Katumba ambako labda rasmi mbio za kuwania ubunge Kyela zitakapotangazwa kuwa ndiyo zinaanza!
Mchukia Fisadi said:
Mpita njia swala hili nilimuuliza mimi na naona anakujibu wewe. Nilijua huyu au anazungumza asichokijua kwa ushabiki wa Yanga na Simba au katumwa aseme PR hapa.
Ni vema katubu na kusema ukweli wote.
Kwa sababu hiyo naomba achangie mengine lakini kwa habari ya Zito anyamaze. Asidandie treni😀ataaibika bure.
Kwa taarifa yake Tanzania Yote shida zetu ni moja hata kama mbunge mnalala naye chumba kimoja🙁 Maana hakuna duka la mbunge peke yake. Hakuna barabara ya mbunge peke yake na hakuna maji ya mbunge peke yake. Hakuna umeme wa mbunge peke yake. Nk,nk,nk,nk,nk,nk.
kwani ulitegemea pinda aseme vinginevyoMpita Njia,
NB:
..habari kwamba Zitto amelitekeza jimbo lake zilianza kutolewa na waziri mkuu Pinda bungeni.
..vilevile kuna mchangiaji wa jamii forums namheshimu sana naye alidai mambo jimboni kwa Zitto siyo mazuri.
Mkuu Heshima mbele sana,
- Kwa taarifa yako ni kwamba muda mchache uliopita ndio kwanza finally, George amefika Kyela kwa gari akitokea Dar, ambako alikuwepo jana baada ya kumaliza matembezi yake ya likizo kwenye mbuga za wanyama, Arusha na nyumba za makumbusho Zanzibar.
- Amekwenda Kyela, yaani nyumbani pamoja na mengine ni kusalimia familia yake na kupumzika kidogo kwa angalau wiki moja, kabla hajaondoka kuelekea Dar na mwishowe UK, anaikoishi na kufanya kazi na familia yake, yaani mke na watoto wake.
- Tunajaribu kuwa on top of this ishu kuepusha majungu tu, nothing of a big deal kuwepo kwake Kyela na likizo yake nzima kwa ujumla. Ya kugombea ubunge ni mpaka yeye mwenyewe atakaposema wazi kama kweli anayo hiyo nia, kitu ambacho sio kuvunja sheria ya Jamhuri kama tunavyotaka kuaminishwa na baadhi ya wenzetu hapa, kama ambavyo pia sio a crime kuwepo huko Kyela kiroho as you reported before, au?
Respect.
Kamanda FMeS!
Malafyale uliandika:
Mwakalinga Awasili Kyela Kumuangusha Dr Mwakyembe
George Mwakalinga mwana Kyela aliyekuwa anaishi na kufanya kazi kama mtaalaum wa kompyuta nchini UK amewasili Kyela majuzi na tayari ametangaza kuwania ubunge wa wilaya ya Kyela ndani ya CCM!
Mwakalinga ametoka kuongea na wana Kyela sasa hivi kwenye hotel ya kisasa ya Sativa na watu waliokuwepo hapo wanasema hapana shaka Mwakalinga kaletwa Kyela na vigogo ndani ya CCM na serikalini na dhahiri anaungwa mkono na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mzee Mwakalinga na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Japhet Mwakasumi!
Mwakalinga,ambae pia ana vitege uchumi vingi sana wilayani Kyela zikiwemo hotel kubwa za kisasa tayari yupo Kyela,na kaanza kuzunguka kwa kasi vijijini kujinadi kwa wana CCM na kuna kila ukweli kuwa viongozi wa CCM wilayani na mkoani wamebariki kuanza huku kwake kampeni kabla ya muda wake.
Kuna madai kwa wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini hawana imani na Mbunge wao, Kabwe Zitto hivyo huenda atalazimika kufanya kazi ya ziada ili abaki kwenye nafasi hiyo.
Inadaiwa kuwa, wapiga kura jimboni humo hawana imani na Zitto kwa kuwa tangu achaguliwe mwaka 2005 hajawasaidia.
Wapiga kura hao wametoa maelezo hayo walipozungumza waandishi wa habari kutoka chama cha waandishi wa Habari mkoa Kigoma waliokuwa wakifanya ziara ya mafunzo kwa vitendo katika vijiji mbalimbali vya jimbo hilo wakati wa mafunzo yao ya uandishi wa Habari za vijijini yaliyofadhiliwa na baraza la Habari Tanzania (MCT).
Wamesema,tangu Zitto achaguliwe mwaka 2005 kuwawakilisha bungeni,hawajawahi kumuona hata mara moja wakimaanisha kwamba, hajawahi kuwatembelea kusikiliza shida zinazowakabili, na pia hakwenda kutoa shukurani kwa kumchagua kuwa Mbunge wao.
Mkazi wa kijiji cha Bitale, Muyera Yahya amewaeleza waandishi wa habari kijijini hapo kuwa Zitto anapaswa kwenda na hoja nzito kuwashawishi wananchi wa kijiji hicho kumchagua tena kuwa Mbunge.
Yahya amesema, Zitto badala ya kwenda kufahamu matatizo yanayowakabili na kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi, amekuwa akizungumzia hoja za Buzwagi ambazo hazina umuhimu wowote kwao.
Mkazi wa kijiji cha Chankabwimba, Kayla Mussa, amedai kuwa,hata katika ziara za viongozi wa kitaifa wa serikali Mbunge huyo hashiriki, viongozi hao wamekuwa wakiambatana na wabunge wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini Peter Serukamba.
Hivi Karibuni Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Kigoma maalum kwa ajili ya kuweka mawe ya msingi ya ujenzi wa barabara za Mwandiga Manyovu na Kigoma Kidahwe kiwango cha lami, na katika ziara hiyo takribani wabunge wote mkoani Kigoma walihudhuria isipokuwa Zitto na Manju Msambya.
Sehemu kubwa ya Barabara hizo zinapita katika jimbo la Kigoma Kaskazini na kwa muda mrefu mbunge huyo alikuwa akisema kuwa yeye ndiye aliyepigia debe hadi serikali kutafuta fedha kwa ajili ya miradi hiyo.
Wakati akiwa katika ziara hiyo,Waziri Mkuu alishangaa kutomuona mbunge wa jimbo la Kigoma kaskazini ,Zitto kwa kuwa miradi hiyo ipo jimboni kwake, wabunge wengine wa mkoani humo walihudhuria.
Waziri Mkuu alisema, kama ni bungeni hata yeye alikuwa huko na wabunge wengine alioambatana nao walitoka bungeni Dodoma hivyo alishangaa kwa nini Zitto hakuwapo na akahoji kama suala hilo halimuhusu.
Hivi karibuni, Pinda alimweleza Zitto bungeni kuwa, kama anataka kuendelea kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini itabidi afanye kazi ya ziada.