ZItto aonesha udhaifu kiuongozi

ZItto aonesha udhaifu kiuongozi

gcmmedia

Member
Joined
Jul 19, 2024
Posts
34
Reaction score
75
Wakati Tundu Lisu anatangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CDM taifa, muda mchache baadae Zitto Kabwe kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, hasa ukurasa wake kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) ameonesha kufurahishwa siyo na kitendo cha Lisu kugombea, Bali kwamba kuna kutokuelewana ndani ya CDM, na labda CDM ndiyo inakufa .

Inawezekana akawa sahihi kuwa huu ukawa mwanzo wa mgogoro mkubwa utakaopelekea CDM kudhoofika na ama hadi kufa kabisa. Lakini hata hili likitokea haliwezi kupiga ya ACT kupata nguvu kubwa na uungwaji mkono mkubwa kufikia hatua waliyofika CDM sasa kuelekea uchaguzi Mkuu mwakani.

Kiongozi mzuri ambaye Ana ndoto za kuwa Rais wa nchi (Kama ZZK mwenyewe ambavyo amekuwa akieleza nia yake hiyo) asingetakiwa kuonesha tabia hiyo. Hii ni dalili kuwa ZZK siyo kiongozi anayeweza kuunganisha Taifa, Bali kushabikia mitafaruku ili afurahie mafanikio yake, ama, anafurahia kisasi kutokea. Ameonesha adui yake Mkuu kisiasa ni ama FAM au CDM.

Angeendelea kipambana kujenga Chamazi ACT

Ngoja inyeshe tuone panapovuja
 
Wakati Tundu Lisu anatangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CDM taifa, muda mchache baadae Zitto Kabwe kupitia Jurassic zake za mitandao ya kijamii, hasa ukurasa wake kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) ameonesha kufurahishwa siyo na kitendo cha Lisu kugombea, Bali kwamba kuna kutokuelewana ndani ya CDM, na labda CDM ndiyo inakuja.

Inawezekana akawa sahihi kuwa huu ukawa mwanzo wa mgogoro mkubwa utakaopelekea CDM kudhoofika na ama hadi kufa kabisa. Lakini hata hili likitokea haliwezi kupiga ya ACT kupata nguvu kubwa na uungwaji mkono mkubwa kufikia hatua waliyofika CDM sasa kuelekea uchaguzi Mkuu mwakani.

Kiongozi mzuri ambaye Ana ndoto za kuwa Rais wa nchi (Kama ZZK mwenyewe ambavyo amekuwa akieleza nia yake hiyo) asingetakiwa kuonesha tabia hiyo. Hii ni dalili kuwa ZZK siyo kiongozi anayeweza kuunganisha Taifa, Bali kushabikia mitafaruku ili afurahie mafanikio yake, ama, anafurahia kisasi kutokea. Ameonesha adui yake Mkuu kisiasa ni ama FAM au CDM.

Angeendelea kipambana kujenga Chamazi ACT

Ngoja inyeshe tuone panapovuja
Vyama vya siasa vyote wangekuwa real na passion ya pamoja leo hii CCM ingekuwa history kama KANU ya Kenya. Wangeungana, lakini ni kutumika na kusaliatiana tu.
 
Tatizo la vyama vinavyojiita upinzani ni kushindana wapo kwa wao badala waungane kumkabili zimwi CCM.
 
Hayo ni mawazo yake binafsi
hata hivyo ulitakiwa ukopy na kupaste hapa alichokiandika na sisi tuone, kwani wengine huwa mnapotosha...
 
Back
Top Bottom