Zitto Kabwe aliwafanyia kitu gani CHADEMA?

Kama senior nyerere alikubali chadema ni habari ya Tanzania na dunia wewe hapa jamiiforum hatapicha yako haipo unatoa ushauri
 
Zitto huyu huyu wa kasulu umweke kundi la upinzani.......!


Jack Zoka akikusikia atacheka mpaka kugala gala chini.
 
Kwani uwepo wa maalim seif ndio ulifanya Act kutokuwa mamluki wa ccm kama ambavyo sasa mnavyoiona?

Wapemba kwa asili sio wafuasi wa ccm, Maalim Seif alikuwa rais mfano halisi.

Na hakuna ubishi Maalim Seif alikuwa mpinzani wa kweli wa ccm.

Hawa wengine hawana misimamo bayana kama ilivyokuwa Maalim Seif hivyo ni rahisi kuburuzwa na Zito kwa ushawishi wa vyeo.

Na fedha.
 
We sema kama umeandika kumtafutia kiki tu otherwise sioni lamaana kwenye bandiko lako.

Zito anajiegemeza ccm ndio mana angalau anaongeaongea vinginevyo zito ni kama Mrematu.

Ukisema chadema wanaongoza wabunge kuhama unawafananisha na chama gani ambacho wabungewke awahami.
 
Chadema ya zamani si ya sasa, wooooote ni wamefikia mahali ni Asante Mhe. Rais., mbowe alichukua muda tu kidogo lakini tunasema wote ni jora moja., Sasaiv mbowe na Lissu wanaeza kwenda Ikulu muda wowote mama akiwaita

Watanganyika hawaaminiki
 
Zitto unamtambua wewe ambaye unapata shibe kupitia kwake.
 
Sasa mpinzani wa kweli angeenda chama ambacho ni mamluki wa ccm?

Mbona inashangaza?

Au ndio maana akakubali na kile cheo ambacho mlitegemea atakikataa?
 
Zitto aliwafanyia nini CHADEMA? Labda kama ni mgeni wa siasa za Tanzania.

CHADEMA ndio walimtengeneza Zitto, lakini baadae akageuka kirusi ndani ya chama. Yeye na watu wake Kitila, Mwigamba, Mchange et al; wakataka kuleta sintofahamu kwenye chama. Wakashughulikwa watumwa wake, na baadae akashughulikwa yeye.

Kazi yake ya kuvuruga mchakato wa kuleta mabadiliko Tanzania bado anaendelea nayo huko aliko. Kwa kifupi, Zitto ni kirusi kwenye safari ya mabadiliko.

Leo anaingia kwenye kama Kamati ya Mukandala! Profesa ambaye hakuna asiyejua itikadi na malengo yake. Prof aliyesema uchaguzi wa 2020 ulikuwa free and fair.
 
Sasa mpinzani wa kweli angeenda chama ambacho ni mamluki wa ccm? Mbona inashangaza? Au ndio maana akakubali na kile cheo ambacho mlitegemea atakikataa?

Toka ameondoka ccm hajawahi kurejea. Labda unamzungumzia Maalim Seif wa Ngamiani.
 
Toka ameondoka ccm hajawahi kurejea. Labda unamzungumzia Maalim Seif wa Ngamiani.
Kwani Zitto yupo ccm au mnasema anatumika na ccm? Sasa na Maalim seif ilikuaje akaenda kujiunga na mamluki wa ccm na tena akakubali cheo ambacho mlitegemea hatokikubali kwa sababu ya kilichotokea kwenye uchaguzi ila wapi Maalim aliamua kukikubali hicho cheo.

Sasa sijui ni nini unataka kutetea wakati kila kitu kipo wazi, Maalim aliungana na mamluki wa ccm na mwishowe akapewa cheo na akakikubali ni sawa vilevile Lissu alivyomsema Anna Mgwila kwamba alipewa zawadi ya cheo baada ya kutekeleza kazi ya ccm.
 
Tatizo la ZITO ni kuwadhidi akili CDM wote....ZZK ana akili nyingi kuliko chadema wengi....

Leo humu CDM wanamuita ZZK ndumilakuwili wanasahau ile issue ya Lowassa na kumsaliti kamanda wao Dr Slaa ndio inawafanya ndumilakuwili namba moja duniani..

Kila siku CDM mnapokea masalia kutoka CCM na watu wenu wengi kila siku wanakimbilia CCM tena wenye hadhi na nyadhifa halafu bado mnamuita ZZK CCM...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…