Zitto Kabwe aliwafanyia kitu gani CHADEMA?

Chadema huwa haikosei kila inachosema na kufanya siku zote huwa ni sahihi tu, na upinzani ndio wenye akili nchi hii na ukizingatia chadema ndio chama pekee cha kweli cha upinzani Tanzania na vyengine vyote ni mamluki tu wa ccm.
 

Maalim sasa alijiunga na ACT akiwa na full control ya huko Zanzibar, hajawahi kuwa na moto sana na huku Bara.

Hicho cheo alichopewa kilikuwa na power zote, na hakuna lolote Zito angeweza kuamua bila Maalim Seif kukubali.
 
Maalim sasa alijiunga na ACT akiwa na full control ya huko Zanzibar, hajawahi kuwa na moto sana na huku Bara. Hicho cheo alichopewa kilikuwa na power zote, na hakuna lolote Zito angeweza kuamua bila Maalim Seif kukubali.
Tuwekane sawa hapa, hivi wakati Maalim seif alipoamua kujiunga na Act alijua kwamba Act ni mamluki au hakujua? Kama alijua kulikuwa na sababu gani ya msingi ya yeye kulazimika kujiunga na mamluki kwani chadema hakuiona ambayo si mamluki?

Au Maalim seif hakuwa akitambua kwamba Act ni mamluki? Au kwamba alijiunga na Act ili tu apate nafasi ya kugombea urais zanzibar na hakuwa akijali kuhusu umamluki wa Act?

Na vp kuhusu cheo alichopewa ambacho mlitegemea kwamba hatokikubali na ataonesha upinzani wa kweli kwa kukikataa ila mwisho wa siku akakubali kile cheo, je hili unalizungumziaje?
 

Kwa taarifa yako nguvu aliyokuwa nayo Maalim Seif asingeweza kuipata akiwa cdm, hivyo akatafuta chama ambacho atakuwa na maamuzi nayo.

Hicho cheo unachosema tulidhani atakikataa Kwanza mimi sio mmoja wa dhana hiyo.

Hata hivyo cheo alichopata bado alikuwa na maamuzi kuliko huyo Zito.

Na ndio maana Zito Membe agombee urais, lakini Maalim Seif alimgomea na kumtaka Lisu.
 
Una maanisha Chadema kuna wenyewe hivyo isingewekana mafahari wawili kukaa pamoja ndio maana akaona bora aungane na mamluki wa ccm na kweli alifanikiwa kupata cheo.

Kiujumla unachoeleza ni kwamba Maalim alikuwa anaangalia masilahi yake binafsi.
 
Zitto kasoma uchumi na anajua ni wapi serikali inakosea kwenye uchumi, wanachadema wengi ni wanasiasa ambao shida yao ni vyeo tu.
 
Una maanisha Chadema kuna wenyewe hivyo isingewekana mafahari wawili kukaa pamoja ndio maana akaona bora aungane na mamluki wa ccm na kweli alifanikiwa kupata cheo.

Kiujumla unachoeleza ni kwamba Maalim alikuwa anaangalia masilahi yake binafsi.

Nguvu waliyonayo cdm hata bila ushirikiano na yoyote wanajimudu. Maalim Seif angejikuta kwenye sehemu ngumu kuwa na maamuzi aliyokuwa nayo ACT. Na kwa taarifa yako kuna ACT na Zito, maamuzi ya ACT yanafanywa na wapemba, ila Zito kwakuwa ndio mwenye chama huwa ana ajenda zake toka kwa waanzilishi halisi wa ACT ambao ni JK, Membe, Mwigulu, Januari, Nape nk. Maalim Seif aliweza kwenda ACT kwani ni chama kidogo, na kiongozi wake ni muislamu tofauti na ilivyo Nccr, TLP, UDP nk. Hivyo kutokana na muda kuwa umeisha asingeweza kuanzisha chama, hivyo ilibidi atafute chama kilicho tayari, ndio zali likawaangukia ACT. Hao wanaccm wafadhili wa ccm Maalim Seif alijua atawadhibiti akiwa ndani, mfano alivyomdhibiti Membe na Zito hakufanya lolote.
 
Kosa la Zitto nakumbuka ilikuwa tetesi za kuutaka uenyekiti wa CDM. KUANZIA HAPO AKAITWA MAMLUKI WA CCM

YANI PALE CDM UKIUTAKA UENYEKITI UNACHUKIWA VIBAYA
 
Kwahiyo Chadema angeshindwa kudhibiti ambayo angeona si sawa ndio maana ukasema asingekuwa na nguvu chadema ambayo alikuwa nayo Act, hapo umenikumbusha sakata la Maalim na Lipumba.

Halafu kumbe ni kweli kwamba Chadema kinaonekana ni chama cha kikristo ndio maana Maalim hakuweza kwenda wapemba wasingemuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…