Zitto Kabwe aripoti Akiwa JUBA sasa hivi

Zitto Kabwe aripoti Akiwa JUBA sasa hivi

The Emils

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
568
Reaction score
124
Zitto Kabwe: Am in Juba-South Sudan, Karibia hotel zote ni 'makeshift' hapa Juba. Baadhi ni containers. Mji umepambwa na picha za Garang. Ulinzi ni wa Hali yajuu sana. V8s, Hummers na Nissan Patrols kila mahala(very unfortunate). Matumaini ya Raia ni makubwa
 
Kama siielewi vile!najua kesho wasudan Kusini wanajitangazia rasmi,ila hii taarifa kama vile haieleweki
 
It will be interesting to know Zitto alienda Sudan ya Kusini kuiwakilisha kambi ya Upinzani, au bunge kwa ujumla wake au Tanzania as a nation? Kama ni kambi ya Upinzani, kwa nini yeye na sio Wenje ambaye ni Shadow Minister for Foreign Affairs?
 
Anyway Zitto unataka kutufahamisha habari ya hotel na Magari or just kututaarifu kuwa upo Juba? Sijakuelewa bado!!! Hebu tufahamishe na maisha ya watu wa hapo Juba na Matarajio yao baada ya kujitangazia uhuru, pengine na business opportunities ambazo waTZ wanaweza kunufaika nazo.

Stori za Hammer na Hotel achana nazo hazitusaidii sana hapa.
 
Usisahau ujana maji ya moto,hiyo ni taarifa cha kuwa yuko huko,sasa kuanzia hapo anza kuuliza maswali ya msingi kwa maono yake kupitia mazungumzo yaka na wasudani hao,nini nafasi ya Tanzania kushirikiana na wadau hao wapya kama Taifa jingine jipya baada ya miaka mingi sana mara baada ya Namibia,Angola na South Afrika Kuwa huru.Tutegemee nini,Je watanzania waangalie maeneo yapi ya uwekezaji yaani ni fursa zipi zinalipa,ujenzi,mawasiliano,mabenki,viwanda na usafirishaji nk.

Toa michongo kupitia tathimi za haraka haraka sana.
 
Wenzeni wa EA wameanza kwenda huko na kutengeneza nafasi za kujasiria mali toka mwaka jana! Kwa sasa sidhani kama kuna nafasi tena!
Niliwaaandikia hapa mapema kuwa Sudani ya kusini wenzenu Wakenya, Waganda na Wanyagwesi wameshaanza kujikita huko lakini sisi tuko kwenye ushabiki maandazi bado!!

Kisha mwisho wa siku tutakuja kusema hapa EA haituthamini!
Wenzetu wanatoka kutafuta nafasi, sisi tunasubiri nafasi zije!!!
Ndio maana migodi yetu inajaa wageni kisha wasomi wetu wanalalamika hawapati ajira!!
 
Hebu fikirieni:

Wakenya wengi wameenda kule kwa ajili ya kufundisha lugha haswa kiswahili! (kiswahili gani!?)
Kuna kazi kuanzia za ushoni, udobi, uhandisi, ushauri, udaktari, uuguzi na ghasia zinginezo ikiwemo umachinga!!
Lakini aaaah! wenzetu mabasi yapo pale kila siku Nbi-Juba. Kigali-Juba, Kla-Juba huku kwetu hakuna...!!! Tunasubiri Serikali iseme!!! na Serikali yenyewe hii hii!!
 
kwa wanaoliza hii habari vipi please tembelea Zitto Kabwe kwenye facebook utaona status yake saa 7 mchana alivyoandika hiyo habari akisema yupo Juba
 
Huwezi amini wako Watanzania Wataalamu wa miamba huko DRC wanaishi kama wafalme na wanalipwa vizuri kwao ajira si tatizo wanaweza kubadili kampuni kama mashati wameshajenga cv kule... lakini waliwahi!!
Walioogopa kutoka bado wanasaga lami katika majiji yetu kana kwamba utaalamu wao unatakiwa mahali kusiko na migodi!!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
nimewahi kufika juba na kukaa huko......hayo magari unayosema hayako mengi kiasi hicho...nchi ile ni maskini sana.labada yawe yamekuja na wageni waalikwa toka nchi za nje kwa njia ya bara bara......
 
wakenya wameshika biashara zote kubwa....hasa biashara za usafirishaji, vifaa ya electronics nk.waganda wao wamshika biashara za nguo na baadhi ya wakenya wanafanya biashara hii....wakati watanzania wafanya biashara walio kule ni wamasai wakiuza dawa za kienyeji.......
 
Yaani huwezi amini, tunawakilishwa na wamasai amabo nawaona ni wajasiri na wanajituma! nimeona makala TBC 1 nikaumia, waTZ nani ametuloga????
 
Nilifika huko mwaka jana, hata biashara ya maji huko ni dili, imeshikwa na wakenya. Malori na hata pick up wanatumia kusambaza maji.
 
Usisahau ujana maji ya moto,hiyo ni taarifa cha kuwa yuko huko,sasa kuanzia hapo anza kuuliza maswali ya msingi kwa maono yake kupitia mazungumzo yaka na wasudani hao,nini nafasi ya Tanzania kushirikiana na wadau hao wapya kama Taifa jingine jipya baada ya miaka mingi sana mara baada ya Namibia,Angola na South Afrika Kuwa huru.Tutegemee nini,Je watanzania waangalie maeneo yapi ya uwekezaji yaani ni fursa zipi zinalipa,ujenzi,mawasiliano,mabenki,viwanda na usafirishaji nk.

Toa michongo kupitia tathimi za haraka haraka sana.

..huko ulikoanzia harakati za ukombozi namibia, angola nk umewekeza nn?? acha ndoto za mchana ww! kapike majungu kuhujumu vyama vya siasa, ndo kazi mnayoiweza uwt wa tz
 
Kama Mh. Zito ameona hayo ndio mambo ya kututaarifu basi safari yetu ni ndefu sana. Infact bado hatujaanza kabisa!
 
Back
Top Bottom