Zitto Kabwe aripoti polisi Lindi, atakiwa kurejea tarehe 20 Julai

Zitto Kabwe aripoti polisi Lindi, atakiwa kurejea tarehe 20 Julai

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Leo tarehe 01 Julai 2020, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe na viongozi 7 wa Chama wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Lindi kama walivyohitajika.

Kiongozi wa Chama na viongozi hao pamoja na Mbunge wa Kilwa Kusini aliyemaliza muda wake Ndugu Suleiman Bungara walikamatwa na Polisi Wilayani Kilwa tarehe 23 Juni 2020 kwa kile ambacho Polisi walikiita "kuhatarisha amani".

Viongozi hao wametakiwa kuripoti tena Polisi Lindi tarehe 20 Julai 2020.

ACT Wazalendo tunaamini kwamba Jeshi la Polisi linatumika kisiasa kuzuia shughuli halali za kisiasa za ACT Wazalendo na kumpotezea muda Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe.

Hivyobasi, ACT Wazalendo hatutarudi nyuma kwenye shughuli zetu za kisiasa licha ya vitisho vya Jeshi la Polisi. Jana Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe amerejea Kilwa kuwapokea madiwani na kufanya kikao na viongozi na Wanachama wa ACT Wazalendo wa majimbo ya Kilwa Kaskazini na Kilwa Kusini. Ziara hizi zitaendelea sehemu nyingine mbalimbali za nchi licha ya vitisho vya Jeshi la Polisi.

Janeth Rithe, Naibu Katibu wa Kamati ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.

1593592593965.png
 
Safari za kwenda Lindi kila baada ya wiki mbili mpaka baada ya October

Atajuta nani alimtuma kuhatarisha amani kwa kupiga honi mfululizo kwny mapokezi yake

Mwana kuli find mwana kuli get
 
Back
Top Bottom