Zitto Kabwe awa mbogo, awashukia vikali wanaodai Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ni Mrundi

Nakuunga mkono
 
Jana nilimuona Abdul Nondo akiongea kwenye media kwa mtindo wa "kufoka foka" huku dada aliyekuwa pembeni akimuangalia kwa mshangao....
Drama za wanasiasa njaa wa enzi za JK zimeanza kurudi kwa mbali!
Mnataka muendelee kuachwa muongee nyie peke yenu? Kina Katambi, Kafulila, Waitala, Lijualikali ..... Siku hizi sio wanasiasa uchwara? Unataka tuendelee kugokewa na kina Polepole?
 
ZIto na kigogo yao mamoja. Asijibalaguze bila sababu kwanza uraia wake ni wa mashaka kuliko Mpango. Hakuna Muha anayeitwa Kabwe!
Kigoma kuna Makabila mengi, Kuna Waha ambao ndiyo kabila kubwa lakini pia kuna Wabembe, Wabwali, Wagoma, Walagarasi na wasukuma (pembezoni)
 
Hoja ya uraia ni mbaya sana. CCM wanaitumia sana kuumiza watu.

Sasa cha kushangaza hata wanaojifanya watetezi nao wanapita njia ile ile. Na waathirika wakubwa ni watu wa mipakani haswa wanaojihusisha na siasa.
 
JF, siku hizi ndiyo maana wakongwe wanachugulia na kuondoka bila kuchangia chochote, uzi kama huu kweli utapata wapi watu makini wa kuchangia labda wazee wa mipasho.
Andika wewe vitu vya maana..kwa Nini nyie mnaojiita wakongwe mna mbwembwe Sana..mnafikiri msipochangia kwenye mijadala ya JF hakuna la maana litakalojadiliwa.

Muda unasonga mbele..lazima maisha yaendelee..wewe endelea kujificha na ukongwe wenu waache vijana waandike kile unachoita mipasho..
 
Hoja ya uraia ni mbaya sana. CCM wanaitumia sana kuumiza watu.

Sasa cha kushangaza hata wanaojifanya watetezi nao wanapita njia ile ile. Na waathirika wakubwa ni watu wa mipakani haswa wanaojihusisha na siasa.
Ni kweli, But, Zito angeweza kumtetea Dk Mpango bila kuhusishwa na Kigoma. Nyerere alitengeneza Tanzania kua kitu kimoja. Ndio maana hata wanaohoji hawasemi kwa nini anapewa umakamu wa Raisi anayetokea Kigoma.

Zito ni public figure asingekua anasema hadharani kua sisi wa Kigoma tutamlinda Dk Mpango. Dk Mpango atalindwa na Tanzania na sio Kigoma.
 
Zitto ni Mfanyabiashara ya Siasa. Yy ni maslahi binafsi kwanza.
 
Watu wa mikoa ya pembezoni huwa wananyanyapaliwa sana kwa kubambikiwa uraia wa nchi jirani.

Zitto yuko sahihi kukasirika
Kwa nini wachaga,wapare,wamasai hawanyanyapaliwi kama waha? Licha ya kuwa karibu na Kenya. Waha ili wasafiri kwenda sehemu yoyote TZ wanatakiwa wawe na barua ya mwenyekiti au kitambukisho.
 
Dr Mpango angefanya kama alichofanya Obama. Aonyeshe cheti chake cha kuzaliwa hadharani. Kesi inakuwa imejifia yenyewe.
 
VP haweza kujieleza kwa upumbavu wenu. Tatizo huyo Kigogo hata hajui lolote kuhusu Waha na lugha yao! Kile ni kiha nanile ni ngoma ya kiha, yes huu ni muda wa Waha kaeni lwa kutulia.
VP hana maamuzi yoyote katika maamuzi ya rais anachoweza kufanya ni kushauri tu hivyo mtulize vihere here huko mipakani.
 
Acha umbayuwayu VP ajieleze kwa huo uzumbukuku wenu.?? Mtakuwa mmekosa agenda!
Acheni kupanic kama nguruwe pori...VP haitaji kutetewa kiivyo mi suala la yeye kutoka hadharani na kuulezea umma asili yake hasa ni ipi, Anaongoza taifa lenye makabila 120 tanznia nzima, haongozi tu watu wa kigoma.
 
Tatizo kubwa ni kwamba Kigoma ni wahanga wakubwa mnoo wa hilo suala kutoka a na misimamo ya siasa zao ikifuatia Kagera. Nambie ninmkoa gani wanaopitia hali kubwa kama hii
 
Tatizo kubwa ni kwamba Kigoma ni wahanga wakubwa mnoo wa hilo suala kutoka a na misimamo ya siasa zao ikifuatia Kagera. Nambie ninmkoa gani wanaopitia hali kubwa kama hii
Ila ukumbuke na historia ya Kigoma ni mkoa uliolea wakimbizi kwa muda mrefu, ko kua na wakazi ambao sio raia wa Tanzania ni jambo la kawaida.
Kule Kigoma abiria wanakaguliwa uraia kwenye mabasi jambo ambalo ni nadra kukuta kwenye mikoa mingine. Kuhoji uraia ni jambo la kawaida. Lisifanye kuugawa utanzania, Tuipiganie Tanzania sio makabili.
 
Acheni kupanic kama nguruwe pori...VP haitaji kutetewa kiivyo mi suala la yeye kutoka hadharani na kuulezea umma asili yake hasa ni ipi, Anaongoza taifa lenye makabila 120 tanznia nzima, haongozi tu watu wa kigoma.
Unajua kuwa mkuu wa idara wa halmashauri tu.. unapitia vetting kiasi gani!?

Yaani tukae hapa tuanze kujadili uraia wa VP!? Basi tuvunje usalama wa taifa. Maana watakuwa wamefail miserably.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania hatujawahi kufanya serious operation ya kufukuza watu. Kwanza Tanzania ya Nyerere ilikuwa inaamini kwenye Pan Africanism, imelea na kutoa passport kibao tu kea watu wasio raia.

Zunguka kwenye magodown ya kihindi na kichina, utakuja lundo LA wahamiaji haramu:Wahindi, pakistan, wachina, Yemen.

Au hao kwasababu hawana athari kisiasa ndio maana hatujali ???
 
Tena manyovu!! mpaka unao tenganisha Manyovu na Burundi ni kijito kinacho tiririka maji safi kidogo kuliko mto ng'ombe pale kjtnyma DSM kipindi cha kiangazi! Wakazi wa hapo wanalima Burundi na hujipatia mahitaji yao huko.

Wanaoleana na kuzikana na kisaidiana mahitaji mbali mbali na wala mpaka huo haulindwi.

Swali, utawezaje kuwatofautisha watu hao kwa sura na tamaduni zao?
 
Watu wa mikoa ya pembezoni huwa wananyanyapaliwa sana kwa kubambikiwa uraia wa nchi jirani.

Zitto yuko sahihi kukasirika
Hana USAHIHI wowote ni MNAFIKI TU kama anapigania hill Mbona Kabendera na Yule ASKOFU walipoambiwa Sio RAIA hakuibuka Kuwatetea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…