Zitto Kabwe na ACT-Wazalendo wamekuwa kimya kuhusu Katiba Mpya, kulikoni?

Zitto Kabwe na ACT-Wazalendo wamekuwa kimya kuhusu Katiba Mpya, kulikoni?

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Tangu kuanza kwa vuguvugu la kudai katiba mpya mapema mwaka huu likiongozwa na Chadema, Zitto Kabwe na chama chake cha ACT Wazalendo wamekuwa kimya pasipo kutia neno lolote.

Hivi karibuni Zitto amesikika akishauri mchakato huu lazima uongozwe na wananchi wenyewe si wanasiasa, kwa upande mwingine mwanaharakati wa mitandaoni anayejulikana kama Kigogo wa Twitter aliyekuwa bega kwa bega na Chadema hivi karibuni amewageuka Chadema na kusema ‘Wanajipanga kuanzisha movement isiyohusisha wanasiasa’.

Wiki iliyopita tumemsikia ndugu Yahaya Omary Mpanda aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Temeke 2020 kwa tiketi ya ACT-Wazalendo akitoa tangazo la kuanzisha Movement ya Wananchi na Katiba kifupi WAKA inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi huu.

Kwa matukio haya pamoja na malumbano yanayoendelea mitandaoni kati ya Kigogo na wafuasi wa Chadema, binafsi naweza kujiridhisha kabisa inawezekana WAKA imeanzishwa kwa ushirikiano wa Zitto na KIGOGO wa Twitter ku undermine movement ya CHADEMA ya kudai katiba mpya.

Ready to be corrected.
 
Zitto ameacha kutabirika kwa vitendo na kauli. Mara baada ya uchaguzi ambao yeye na ACT yake pamoja na CHADEMA wslilalamikia ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi alisaini makubaliano na ya kutoshiriki chaguzi zote hadi kufanyike marekebisho waliyoyaanisha. Haikuchukua muda tukamwona kwenye chaguzi ndogo Kigoma na Tunduru.

Kuna wakati akasifu mwenendo wa uchaguzi kuwa ilikuwa huru na haki kisha akageuka na kulalamika kuwa hazikuwa za haki. Wakati CHADEMA wanahanasisha watanzania kutaka katiba mpya yeye yuko busy na siasa za kimataifa hususan Tugrey, Somalia na hivi karibuni Zambia. Ameenda mahabusu jumjulia hali Mbowe ambalo ni jambo jema lakini kajasema chochote kuhusu kile kilichosababisha Mbowe awekwe ndani. Zitto amebadilika na sababu anaijua yeye mwenyewe.
 
Sababu wanajitambua na wanajua nini kiombwe, wakati gani na namna gani. Umewasikia juzi kule Zanzibar baada ya figisu za uchaguzi wa Konde waliomba kuonana na Rais (kwa staha), akawakubalia na walienda kuonana naye (kimya kimya bila makelele ya kwenye press), wakampa malalamiko yao, akawaahidi atayafanyia kazi, haukupita muda mrefu Mbunge wa CCM aliyechaguliwa kajiuzulu na uchaguzi utarudiwa upya. Huo ndiyo uzuri wa kujitambua, especially chama kinapokuwa kinawasikiliza watu wenye busara na uzoefu wa siasa kama Mzee Duni.
 
"Usiwe unaongea wakati unakula" wahenga walisikika wakisema mahali fulani.
 
Sababu wanajitambua na wanajua nini kiombwe, wakati gani na namna gani. Umewasikia juzi kule Zanzibar baada ya figisu za uchaguzi wa Konde waliomba kuonana na Rais (kwa staha), akawakubalia na walienda kuonana naye (kimya kimya bila makelele ya kwenye press), wakampa malalamiko yao, akawaahidi atayafanyia kazi, haukupita muda mrefu Mbunge wa CCM aliyechaguliwa kajiuzulu na uchaguzi utarudiwa upya. Huo ndiyo uzuri wa kujitambua, especially chama kinapokuwa kinawasikiliza watu wenye busara na uzoefu wa siasa kama Mzee Duni.
Hata wakiuawa wakati wa uchaguzi wauawe kimya kimya wasitupigie kelele,

Ndugu yangu kilichofanyika ni bargaining kati ya damu na ubunge au kati ya utu wa mtu na pesa au cheo nothing else.
 
Back
Top Bottom