Zitto Kabwe: Nani anaongoza nchi yetu?

Acha uchizi weye!
Media zote dunia nzima zina taarifa hiyo. Wewe unaishi dunia ipi?
Muda utasema tu.....Acha CCM wabane,wadanganye, watishie watu na kuwaweka ndani but at end of the day they' ll state it clearly.
 
Mimi nina hofu ya kitu kimoja tu, kuhusu upigaji ktk kipindi hiki ambapo raisi hafanyi ziara. Maana wale vigogo wamaweza fanya miamala ya hovyo kabisa kwenye hela za umma
yees hii ndo fursa kwao tena wapige wasiangalie nyuma. Siku akifa wao tayari ni tajiri.
Wanipe mimi niwatunzie huku ughaibuni
 
Zitto bhana! Uambiwe na nani sasa hali ya Rais?

Waziri mkuu kasema yuko fiti
Makamu Rais kasema rais yuko fiti

Unataka uambiwe na nani sasa?

Huu upumbavu kumbe hadi kwa wasomi upo?
KWA KWELI HAPA ILIPOFIKIA NA MUDA ULIOPITA NI SAWA TU KUULIZA MASWALI. AMBAYE HAULIZI NDO WA KUSHANGAWA.

NILIWAAMINI SANA WAZIRI NA MAKAMO ILA KUTOTOKEA KWAKE MPAKA SASA SINA SABABU YA KUAMINI MANENO MATUPU TENA.
 
Hao wooote wanaosema jiwe haumwi ndo wamemroga.km idegenda ni mlozi huyu!wanatupotezea tu.kujifanyafanya tu!
 
Ni dhahiri sasa kwamba Magufuli anaumwa, hilo sio swali tena lenye utata.

Kinachoonekana pia, ni kwamba kuna matumaini ya hali yake kutengemaa na pengine kurudi tena kazini

Kinachosubiriwa tu sasa ni hali yake, apate nafuu..., na mengine yataendelee baada ya hapo.

Hawawezi tena kukana kuhusu hali inayomkabili Magufuli sasa hivi.
 
Sasa kama waziri mkuu keshatoa hilo tamko ina maana Zitto hajui anayeongoza nchi nani? Ni Dk Magufuli aliyeongea na Waziri Mkuu
Waliongea wakiwa wapi? Yani yule mzee aliyewahi kuwapigia simu kina diamondwakiwa kigoma ashindwe kumpigia simu PM tena akiwa amezushiwa KIFO?.labda kama co MAGUFULI mjua yote
 
Nenda you tube msikilize chahali.
 
bado baraza la mawaziri halijaona tatizo lolote ndomaana mpaka leo kipengere hicho cha katiba hakijafuatwa pia kila kitu kiko wazi kwani katika ziara za makamu wa rais au waziri mkuu kuna kipengere chochote cha katiba kimekiukwa?

Pia kipengere hicho cha katiba hakijaeleza ukomo wa muda ambao baraza la mawaziri litaamua kuitisha kikao kujadili afya ya mh.Rais hivyo hakuna ulazima wa kuliforce likutane wakati hakuna tatizo lolote na kila kitu kiko shwari mbona majibu yapo wazi tu
 
Wahusika wenyewe (yaani wanaojiita wahusika) hata mimi siwajui sana kwa sababu ukiuliza yuko wapi wanakuparamia ilie mbaya wakati na wao hawana taarifa.Ila wanaomficha wajue duniani hakuna siri wa zaidi ya mtu mmoja ,ukweli utajulikana tu .Endelea kuangaza angaza unaweza kupata habari huku uku kwani lisemwalo laja
 
Ni jibu zuri..., hasa kuhusu "kipengere cha katiba" kutoeleza ukomo wa muda ambao baraza la mawaziri litaamua kuitisha kikao...

Rais anaumwa, lakini hali yake inaweza ikarekebika na kumwezesha kurudi kazini...., labda?

Hakuna anayeweza kwa sasa hivi kuanzisha taratibu walizozielezea ACT hapo juu katika hali ya namna hiyo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kwa hiyo Lisu anasemaje kafufuka au?
 
Naanza kuogopa kuwa rais wetu,Mungu wangu
 
Kikwete akiwa raisi aliwahi kwenda Uk kufanyiwa upasuaji wa tezi dume na taarufatulikuwa tunapatiwa. mbona la huyu linakuwa gumu?
Kwaiyo we unaamini katika miaka 10 ya Kikwete aliumwa tezi dume tu?? Hakuwah kuumwa kingine chochote? Au kwakuwa iyo ulipe notes yake ndo umeijua?
 
Kwani si tumeoneshwa akiapisha mabalozi juzi tu hapo? Au ilikuwa video ya zamani?
 
Zitto bhana! Uambiwe na nani sasa hali ya Rais?

Waziri mkuu kasema yuko fiti
Makamu Rais kasema rais yuko fiti

Unataka uambiwe na nani sasa?

Huu upumbavu kumbe hadi kwa wasomi upo?
Bado msemaji wa serikali hajasema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…