Suphian Juma
Senior Member
- Apr 2, 2019
- 140
- 577
NUKTA NANE MUHIMU KWA SIKU YA DUNIA YA BIMA YA AFYA KWA MTANZANIA KUTOKA KWA KIONGOZI WA ACT WAZALENDO, ZITTO KABWE.
Leo Desemba 12, 2019 ni siku ya Dunia ya Bima ya Afya kwa wote. Bima ya afya ya Taifa haipaswi kufanywa biashara. Bima ya afya ya taifa inapaswa kutekeleza Sera ya Afya ya Taifa kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata haki ya matibabu. Kuifanya Afya kuwa Bidhaa ni usaliti kwa Wananchi.
Tunaadhimisha siku hii, Watanzania wengi bado hawana Bima ya Afya ya Uhakika. Bima ya Afya ya Jamii ambayo ndio ina watu wengi ina huduma dhaifu sana na inaishia kwenye Zahanati ya Kijiji. Bima ya Afya ya Taifa sasa imegeuzwa kuwa Biashara Kwa watu wenye uwezo tu.
Chama chetu kinapigania kuubadili mfumo wa Hifadhi ya Jamii ili Serikali na Wananchi wachangie kwa pamoja ( matching scheme) na Fao la Afya kuwa kwa wote bila kujali kiasi cha mchango wake (contribute according proportionate to income, access according to needs).
ACT wazalendo ITAPITIA upya sheria iliyoanzisha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kumwezesha na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na haki ya matibabu na huduma za afya kupitia mfumo wa umma.
ACTwazalendo ITATUNGA sheria itakayopelekea Serikali kuchangia angalau theluthi moja ya kila mchango wa mwananchi atakayechangia kima cha chini cha michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na hivyo kuwezesha Wananchi kuwa na Bima ya Afya ISIYOBAGUA aina ya matibabu.
Takwimu za Hali ya Uchumi wa Taifa ya mwaka 2019 inaonyesha mwaka 2018 Watanzania 41 milioni walikuwa wagonjwa wa nje kwenye Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati Nchi nzima. Hii ina maana kuwa 77% ya Watanzania waliumwa mwaka 2018. 91% ya hawa hawana Bima ya Afya.
Tunataka taasisi yetu ya NHIF isichepuke kutoka kuwa Skimu ya Bima ya Afya ya Umma. Viwango vya Michango viendane na uwiano wa kipato cha Mwanachama na Mafao yawe sawa kwa watu wote bila kujali kiasi cha mchango. Hii ndio kanuni ya msingi ya Bima ya Afya ya Umma.
NHIF haizuiwi kuanzisha Kampuni Tanzu ya Bima ya Afya ili kufanya Biashara ya Vifurushi. Huduma kutolewa kwa kuzingatia kifurushi ni kitendo cha kuifanya NHIF kuwa Bima Binafsi na kubidhaisha Afya ( commoditization of health ). Huo ni wajibu wa sekta binafsi.
Imetolewa na;
Suphian Juma,
Afisa Habari, ACT wazalendo
Desemba 12, 2019.
Sent using Jamii Forums mobile app