Zitto Kabwe, Pemba sio Kigoma

Zitto Kabwe, Pemba sio Kigoma

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Jana tumeshuhudia maziko ya Mwanasiasa mkongwe yaliyofanyika huko Pemba Zanzibar kijijini Nyali Mtambwe na kuona jinsi wananchi wa huko walivyokuwa na simanzi nzito mithili ya kuwa wameondokewa na mfalme wao. Na wengi walionekana kama kuwa sasa ndio basi tena hakuna wa kuja kuwapigania. Maana nilisikia baadhi ya watu wakizuiwa kulia ili wasije kukufuru.

Ni wazi kuwa kwa wapemba Maalim Seif wao walimchukulia kama mkombozi, hata kama angerudi CCM basi Pemba ingerudi kuwa ngome ya CCM.

Sasa ameondoka, hivi kwa akili ya kawaida Zitto anaweza kuwa na ushawishi huko Pemba kiasi cha kutuliza mizuka ya Wapemba?

Pemba tunaiijua tangu mwaka 1995 ulipofanyika uchaguzi mkuu wa vyama vingi ni Maalim Seif alikuwa akituliza hasira za Wapemba ambao kwao wanaona kama wanakandamizwa kwa kila namna.

Tusisahau kuwa hata hata baada ya uchaguzi wa 2000 na machafuko makubwa kutokea ni ushawishi wa Maalim uliosababisha kupatikana kwa muafaka wa kisiasa. Hata maridhiano ya kisiasa yaliyopelekea kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar ni sababu Maalim Seif alitumia ushawishi wake kupoza joto Pemba.

Zitto baada ya kuona mambo magumu huku bara ulikuwa unatembelea mgongo wa Maalim Seif huko Pemba. Na unatakiwa kujua Wapemba sio kondoo kama jamaa zako. Huu ndio mwisho wa janja zako.
 
Najaribu kuwaza kitu gani kimekufanya uandike hii post katikati ya majonzi mengi. Umeshindwa kabisa kuficha chuki yako dhidi ya Zito? kweli mtihani huu.
 
Najaribu kuwaza kitu gani kimekufanya uandike hii post katikati ya majonzi mengi. Umeshindwa kabisa kuficha chuki yako dhidi ya Zito? kweli mtihani huu.
Sidhani kama ni chuki dhidi ya Zitto bali ni ukweli. Kama ni majonzi tunayo wote lakini ukweli tunaambizana.
 
Km ni ishu yakuitaji badiliko inaendlea kuwepo so bado nahisi atakae onyesha nia hasa ya kufit madaliko wanayoyataka wapemba anaweza kupata kundi kubwa coz wapemba ni watu wakuamini jambo na kulisimamia hawayumbi kizembe
 
Kama Seif kafia ACT basi hiyo pia inaweza kuwa blessing kwa Zitto.
]Sio kwa maamuzi yale ya serikali ya kitaifa huwajui wapemba wewe, niulize mimi ni wajomba zangu haswaa toka ntoke na mama yangu nawajua uzuri sana ....

Kama unabisha jaribu kukubaliana jambo lolote na mpemba yeyote mwenye duka lake au banda la chips au genge la kufyatua matofali maeneo yako au hapo mtaani kwako halafu baada kuanza kutekeleza geuka uje na maamuzi mengine uone moto wake !!!

ACT kwisha habari yake tena wapemba wanaanza upyaaaaaaa! Tena muanzaji lazima awe mpemba mwenzao kama unabisha utaona
 
Back
Top Bottom