Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Bado kuna na tozo mkuu, Watumiaji wa mitandao wote zanzibar wanakatwa tozo na Jamhuri, Mitandao ya simu, ma bank, yote yana operate zanzibar huku kodi zao wakiwa wanalipa Bara. watalii wote wanaokwenda zanzibar hela ya visa inaingia kwa Jamhuri.
Hiyo TRA ni chanzo Kimoja tuu ila kuna Utitiri wa Mataasisi yanayokusanya pesa Bara na Zanzibar.

Kiufupi Zanzibar inapinjwa parefu.
 
Zitto ana Siasa za kitoto sana

Lini umesikia Watanganyika wanalalamikia muungano tana G55 ya Akina Njelu Kasaka iyeyushwe?

Tanganyika ni shamba la Wapemba tangu enzi za Sultan 🐼

Asilimia Kubwa ya wakulima wa mpunga Usafwani ni Wapemba 😂

Mzanzibar hela yake kaifata huku huku Bara hana muda wa kusubiri Mgao kama hivyo vihalmashauri vyenu!
 

Kulikuwa na haja gani kudhihirisha Ujing wako? Chuki za kidini zinakuteseni sana wagalatia
 
Huyu chenga tu kwanini asioneshe pia wao wanachangia kiasi gani
Kila siku nunajadili masuala haya lkn hatupati suluhusho kwasababu baadhi ya wachangiaji hawaelewi hata kinachobishaniwa, Kwanza mnatakiwa muelewe kuwa chanzo kikuu cha hayo yanayoitwa 'mapato ya muungano' yanayobishaniwa ni misaada kutoka nje, sio mapato ya korosho, pamba, utalii, bandari n.k. Naamini ungeelewa hili kabla, usingeuliza wao wanachangia kiasi gani.
 
mh...
Hii nchi ambayo ipo kwenye soko huru na Oman,uagizaji vitu kwa kodi nafuu...

Watu hukimbilia huko kununua vifaa vya electronics kisa bei chee...

Bidhaa zipi Zanzibar ni bei ghali, mbona watupiga changa la macho.
wewe huishi Zanzibar, huwa unasikiliza stori za vijiweni tu kwa hivyo endelea tu.
 
Ule uwe mkoa tu maana sisi waTanganyika hatuna mpango wa kuiacha ile ardhi na bahari yake. Ule ni urithi wa baba Nyerere na Karume hauuzwi. Akitokea mtoto anataka kuuza tunamvamia kama nyuki wanavyovamia mvuna asali.
Sasa mbona munalalamika? Kaeni kimya basi pole sana
 
Wewe huna hoja umeandika porojo tu huna ujualo pole sana
 
wewe huishi Zanzibar, huwa unasikiliza stori za vijiweni tu kwa hivyo endelea tu.
Mkuu Zanzibar nishafika,,,
Safari ya kwanza nilifika Chukwani,Safari ya pili nikakaa Airport, kona ya kuelekea baraza la wawakilishi...
Kariakoo kwenye mabembea,Shamba,Fumba,Kwa Mchina nishapita hadi hapo Darajani kwenye Masoko.

Bidhaa nyingi Zanzibar zinatoka Uarabuni...yani hadi Simenti mnaagiza kutoka Uarabuni....

Nenda mikoa ya bara ukajionee bidhaa zilivyogharama.

Acha kupotosha watu....
 
Yeye akiwa Rais atawagawanya bara sawa kwa sawa na visiwani. Je Ratio ya mapato bara na visiwani yakoje?
Huyu msaliti hana jipya! Aulizwe zanzibar wanazalisha nini? Je mapato ya uzalishaji wa zanzibar vinakuja bara! Rubbish
 
Mij
Ndio matajiri wa Bara hapa,punguzeni majungu na fitina pigeni kazi
Mijadala mingi humu inaharibiwa na wapuuzi, hivi kwa mfano suala la swala tano linahusianaje hapa? mimi nadhani suala la kipato cha nchi au mtu binafsi hakihusiani na imani. ndio maana unawezakuta kuna 'swala tano' ana elimu na maendeleo kuliko hata mliberali, tujikite kwenye mada tusijetukaonekana kuwa sote ni wajinga
Kwenda zako wale mamwinyi swala Tano kazi Gani wanaweza?
 
Kwenda zako wale mamwinyi swala Tano kazi Gani wanaweza?
Said Salim Bakhresa, Harun Zakaria, Salim Turky hawa nao ni Swala 5 wa kizanzibar lakini ni moja ya matajiri wakubwa hapa Tanzania unasemaje kuhusu hilo?
Aliyekwambia swala 5 ni wavivu nani?
Karibia matajiri wote wenye majina ndani ya Tanzania ni swala 5.
Sijui kama unalijua hilo!!
Chuki zako za kidini usiingize kwenye siasa.
 
Kwani haujasikia kwenye mikutano yao zile salamu zao kila kiongozi apandapo jukwaani.
Utasikia " Zanzibar........"
Kisha sikia wafusi wake wanavyoitikia.
Hapo ndipo utajua kauli yake ipo kinyume na wanampango wa kuleta chuki zaidi.
Anataka kuwaaminisha wazanzibar kuwa wao hawana faida ya Muungano kwa kupewa 2% na huku akijui chama chake kina nguvu na wanachama wengi Zanzibar.
 
Zitto ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Huyo Zitto naye namna gani tena, kwa serikali ya JMT, Zanzibar ni mkoa tu kwa sababu wana mamlaka yao ya mapato...

Hoja ya Zitto ingekuwa na mashiko kama kungekuwa na kapu moja la mapato, then ingeeleweka kama mgawanyo wa mapato uwe mnono kwa Zenji...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…